Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Je, Unaweza Kupata Upendo wa Kweli? (Machi 2006) Ulimwengu umepotosha maana ya upendo, na Shetani anataka kuuharibu kabisa. Habari kama hiyo inatusaidia kuonyesha upendo kwa matendo na bila ubinafsi. Asanteni kwa kunisaidia kujua zaidi jinsi ambavyo Yehova angependa tuonyeshe upendo.

Y. B., Marekani

Nilihisi upweke marafiki wangu wawili wa karibu walipohama wakatumike katika kutaniko la lugha tofauti. Lakini upweke wangu ulipokuwa tu umezidi, nikapokea gazeti hilo. Asanteni sana kwa kunikumbusha kwamba, “Ukitaka kupendwa, waonyeshe wengine upendo.” Kuanzia leo, ninapanga ‘kupanuka’ na kuonyesha upendo wa kuhisiwa moyoni ili niwe na marafiki wapya.—2 Wakorintho 6:12, 13.

M. T., Japani

Kukabiliana na Matatizo ya Uzee (Februari 2006) Mara nyingine mimi huhisi kwamba wazee wanasahauliwa. Nimekuwa nikimtunza mume wangu asiyejiweza kwa miaka 11 sasa. Mara nyingine mimi huhisi upweke. Nilisoma tena na tena makala hizo katika Amkeni! hiyo na kuzisikiliza katika kaseti mara nyingi sana. Gazeti hilo lilinifaa sana. Asanteni sana.

S. T., Japani

Viungo Bandia (Februari 2006) Asanteni sana kwa makala kuhusu viungo bandia. Nilipokuwa na mimba ya miezi mitatu, tuliambiwa kwamba mtoto wetu angezaliwa bila mikono na miguu na kwamba angepewa miguu bandia atakapokuwa na umri wa mwaka mmoja. Makala hiyo iliwasili mwezi uleule Daryl alipofikisha mwaka mmoja. Sasa anajifunza kusimama na kutembea. Mimi na mume wangu tunatazamia sana wakati ambapo Daryl “atapanda juu kama vile paa anavyofanya.”—Isaya 35:6.

Y. A., Ufaransa

Uhai Una Thamani (Oktoba 22, 2001) Nimesoma Amkeni! la Oktoba 22, 2001, mara nyingi sana, hasa wakati ninapovunjika moyo. Habari hiyo ni kama dawa kwangu lakini habari hiyo haipitwi na wakati. Mashauri na suluhisho linalotolewa kwa matatizo yetu ni lenye manufaa sana. Gazeti la Amkeni! hunitia moyo na kunifanya nihisi kwamba mnajali watu kama mimi. Ninafurahi sana na kushukuru kwamba mnanikumbusha kwamba “uhai una thamani”!

P. T., Madagaska

Mahujaji na Wapuriti—Walikuwa Nani? (Februari 2006) Nilichukizwa na jinsi ukweli ulivyopotoshwa katika makala hiyo. Kuna sababu ya msingi inayofanya Wenyeji wa Asili wa Amerika Kaskazini wasisherehekee Sikukuu ya Kutoa Shukrani, nanyi hamkutaja mambo waziwazi.

Jina limebanwa, Marekani

“Amkeni!” lajibu: Kusudi la makala hiyo haikuwa kuchunguza kwa undani historia ya Sikukuu ya Kutoa Shukrani. Vichapo kadhaa vya marejeo kutia ndani “Encyclopædia Britannica,” vinaripoti kwamba katika mwaka wa 1621, mahujaji walisherehekea kwa siku tatu pamoja na marafiki wao Wenyeji wa Asili wa Amerika. Hili limefafanuliwa katika barua iliyoandikwa na Edward Winslow, mnamo Desemba 11, 1621. Lakini kwa miaka iliyofuata, sikukuu za kutoa shukrani zilitumiwa kusherehekea matukio mengi zaidi ya mavuno. Sherehe inayojulikana zaidi katika historia ni ile iliyotangazwa na Gavana John Winthrop wa Massachusetts Bay Colony katika mwaka wa 1637 baada ya mauaji ya mamia ya Wenyeji wa Asili wa Amerika wa kabila la Pequot. Kwa hiyo, tunaweza kuelewa kwa nini wasomaji fulani wanachukizwa na Sikukuu ya Kutoa Shukrani.