Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Dubu wa Majini Ambaye Hafi kwa Urahisi

Dubu wa Majini Ambaye Hafi kwa Urahisi

Dubu wa Majini Ambaye Hafi kwa Urahisi

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI JAPANI

▪ UKITAFUTA katika mazingira yoyote yaliyo na maji ulimwenguni, kama vile kwenye kuvumwani, barafu, chini ya mito, chemchemi za maji moto, maziwa, bahari, na hata katika bustani yako, unaweza kumpata dubu wa majini, ambaye ni mojawapo wa viumbe wadogo zaidi wasioweza kufa kwa urahisi. Dubu wa majini ni mdogo sana hivi kwamba hawezi kuonekana kwa urahisi. Mwili wake ulio na sehemu nne umefunikwa kwa ngozi ya kumlinda, naye ana miguu minane, kila mmoja ukiwa na kucha. Umbo lake hufanana na dubu anayetembea, ndio sababu anaitwa dubu wa majini.

Dubu wa majini hutembea polepole. Kuna aina nyingi sana za dubu hao. Dubu wa majini wa kike hutaga kati ya yai 1 hadi 30 kwa wakati mmoja. Mkono mmoja tu wa mchanga au udongo wenye maji unaweza kuwa na maelfu ya viumbe hao wadogo. Mahali pazuri zaidi pa kuwapata ni kwenye paa lililo na kuvumwani.

Dubu hao wanaweza kuishi katika mazingira magumu sana. “Walipowekwa katika mahali pasipo na hewa kwa siku nane, kisha wakahamishwa na kuingizwa katika chumba chenye gesi ya heli chenye joto la kawaida kwa siku tatu, halafu wakatiwa mahali palipo na baridi kali ya digrii 272 Selsiasi chini ya sufuri (-458°F) kwa saa kadhaa na mwishowe wakarudishwa katika mazingira ya kawaida, walianza kutenda tena,” kinasema kitabu Encyclopædia Britannica. Pia wanaweza kustahimili miale ya eksirei iliyozidishwa mara mia zaidi ya ile ambayo ingemuua mwanadamu. Na inafikiriwa kwamba wanaweza kustahimili hata wakipelekwa anga za juu mahali ambako hakuna oksijeni!

Kinachowasaidia ni uwezo wao wa kuwa kama wamekufa wakati ambapo wao huyeyusha chakula polepole sana! Ili kuwa katika hali hiyo, wao huingiza miguu ndani ya miili yao na kujikunja kama mpira wenye nta kwa kuwa maji yoyote yanayotoka mwilini hugeuzwa na kuwa sukari. Wanapokuwa tena katika mazingira yenye unyevunyevu wao huanza kutenda tena katika muda wa kati ya dakika chache au saa chache. Katika kisa kimoja dubu wa majini waliokuwa ni kama wamekufa kwa miaka 100, walianza tena kutenda!

Naam, kwa utulivu na njia inayopendeza, viumbe hao wadogo ‘wanaotambaa’ humsifu Yehova.—Zaburi 148:10, 13.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 30]

© Diane Nelson/Visuals Unlimited