Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kituo cha Umeme Chatokeza Mwangaza wa Kiroho

Kituo cha Umeme Chatokeza Mwangaza wa Kiroho

Kituo cha Umeme Chatokeza Mwangaza wa Kiroho

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI ITALIA

▪ Mapema katika miaka ya 1900, viwanda vilianza kusitawi kwenye milima ya Pistoia, huko Italia. Ili kusafirisha mali-ghafi na bidhaa zilizokamilika, reli ya umeme ilijengwa. Reli hiyo ambayo ilizinduliwa Juni 21, 1926 (21/6/1926), ilikuwa nyembamba na ilipita juu ya vilima na milima kwa karibu kilomita 15.

Nguvu za umeme zilizokuwa zinatumiwa kwenye treni hiyo zilitoka katika kituo kidogo cha umeme (juu kushoto). Hata hivyo, mwishowe kupungua kwa biashara kulifanya huduma hizo za reli zipungue na hivyo kituo hicho kikafungwa mnamo 1965. Majengo yaliyokuwa kando ya reli hiyo yalikwenda wapi? Mengine yalianza kuharibika, mengine yakageuzwa kuwa baa na vituo vya basi.

Kituo hicho kidogo cha nguvu za umeme kilirekebishwa. Mnamo 1997 jengo hilo lilinunuliwa na Shirika la Mashahidi wa Yehova la San Marcello Pistoiese na kugeuzwa kuwa moja ya Majumba ya Ufalme yenye kupendeza zaidi ya Tuscany (chini kushoto). Washiriki wa kutaniko linalokutana katika kituo hicho cha zamani ‘wanaangaza kama mianga’ katika maeneo hayo ya mlimani, wakihubiri habari njema ya Ufalme wa Mungu. (Wafilipi 2:15; Mathayo 24:14) Naam, jengo ambalo awali lilitumiwa kueneza umeme halisi linatumiwa kueneza nuru ya kiroho.—Mathayo 5:14-16; 28:19, 20.