Ungejibuje?
Ungejibuje?
NI NANI ALIYESEMA MANENO HAYA?
Chora mstari wa kuunganisha maneno na mtu aliyeyasema.
Musa
Petro
Yohana
Adamu
1. “Watoto wadogo, jilindeni na sanamu.”
2. “Mwishowe huyu ni mfupa wa mifupa yangu.”
3. “Adui yenu, Ibilisi, anatembea huku na huku kama simba anayenguruma.”
4. “Tangu wakati usio na kipimo mpaka wakati usio na kipimo wewe ni Mungu.”
▪ Zungumzeni Pamoja: Ni jambo gani lingine unalojua kuhusu mtu huyo wa nyakati za Biblia?
ILITUKIA LINI?
Taja jina la mwandishi aliyeandika kitabu cha Biblia kilichoorodheshwa hapa chini, na uchore mstari unaounganisha kitabu na tarehe kilipokamilishwa kuandikwa.
1450 K.W.K. 844 K.W.K. 536 K.W.K. 56 W.K. 61 W.K.
5. Danieli
6. Yona
7. Waebrania
MIMI NI NANI?
8. Muujiza ulifanya magoti yangu yagongane.
MIMI NI NANI?
9. Nilimtoroka bwana wangu lakini nilipokuwa Mkristo nikarudi kwake.
KATIKA TOLEO HILI
Jibu maswali haya na utaje mistari ya Biblia ambayo haijaonyeshwa.
Ukurasa wa 5 Mtu asiye na uzoefu hufanya nini? (Methali 14:____)
Ukurasa wa 11 Ni sifa gani hufanyiza kifungo kikamilifu cha muungano? (Wakolosai 3:____)
Ukurasa wa 19 Sisi sote hufanya nini mara nyingi? (Yakobo 3:____)
Ukurasa wa 28 Kifo kilieneaje kwa watu wote? (Waroma 5:____)
Watoto Watafute Picha
Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.
(Majibu kwenye ukurasa wa 14)
MAJIBU YA UKURASA WA 31
1. Yohana.—1 Yohana 5:21.
2. Adamu.—Mwanzo 2:23.
3. Petro.—1 Petro 5:8.
4. Musa.—Zaburi 90:2.
5. Danieli, 536 K.W.K.
6. Yona, 844 K.W.K.
7. Paulo, 61 W.K.
8. Belshaza.—Danieli 5:1, 5, 6.
9. Onesimo.—Filemoni 10-16.