Mfumo Unaoongoza Safari ya Kipepeo
Je, Ni Kazi ya Ubuni?
Mfumo Unaoongoza Safari ya Kipepeo
▪ Akitumia ubongo unaotoshana na ncha ya kalamu, kipepeo anayeitwa monarch anasafiri kilomita 3,000 hivi kutoka Kanada hadi kwenye msitu mdogo nchini Mexico. Mdudu huyo anajuaje njia atakayopitia?
Fikiria hili: Kipepeo huyo hutambua mahali anakoelekea kwa kutegemea mahali jua lipo. Lakini si hilo tu. Wadudu hao pia hutumia utaratibu sahihi sana wa kibiolojia wa saa 24 ili kujipatanisha na mwendo wa jua. Dakt. Steven Reppert, mtaalamu wa mfumo wa neva, anasema kwamba vipepeo hao “wana utaratibu tofauti wa kutambua wakati wakilinganishwa na wadudu na wanyama wengine ambao wamechunguzwa kufikia sasa.”
Kujifunza mengi zaidi kuhusu jinsi kipepeo anayeitwa monarch anavyotambua wakati, kunaweza kuwasaidia wanasayansi kuelewa jinsi wanadamu na wanyama wanavyotambua wakati kiasili. Pia kunaweza kuchochea kuanzishwa kwa matibabu mapya ya magonjwa ya mfumo wa neva. “Ninataka kuelewa jinsi ubongo unavyopokea na kutumia habari kuhusu wakati na mwelekeo,” anasema Reppert, “na kipepeo anayeitwa monarch anaweza kunisaidia sana kutimiza lengo hilo.”
Una maoni gani? Je, mfumo wa kipepeo unaomwongoza anaposafiri ulijitokeza wenyewe? Au unathibitisha kwamba kuna Mbuni mwenye akili?
[Mchoro/Ramani katika ukurasa wa 10]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa
Kipepeo anayeitwa “monarch” anasafiri kilomita 3,000 hivi kutoka Kanada hadi kwenye msitu mdogo nchini Mexico
[Ramani]
KANADA
MAREKANI
MEXICO
MEXICO CITY
[Picha katika ukurasa wa 10 zimeandilwa na]
Background: © Fritz Poelking/age fotostock