Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?

Soma Mathayo 25:1-12. Kisha utazame picha. Kuna kasoro gani? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

4. ․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Kwa nini mabikira watano hawakuwagawia wenzao mafuta?

DOKEZO: Soma Mathayo 25:8, 9.

Ni wakati gani inapofaa kuwagawia wengine vitu tulivyo navyo? Ni wakati gani ambapo haifai kuwagawia wengine vitu tulivyo navyo?

Katika Toleo Hili

Jibu maswali haya na utaje mistari ya Biblia ambayo haijaonyeshwa.

UKURASA WA 6 Ni nani anayeimiliki dunia na vitu vinavyoijaza? Zaburi 24:________

UKURASA WA 9 Mtu yeyote aliye na kiu anaweza kupata nini? Ufunuo 22:________

UKURASA WA 18 Mtu mwenye utambuzi ana nini? Methali 17:________

UKURASA WA 29 Upumbavu wa mtu unaweza kufanya nini? Methali 19:________

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Unajua Nini Kuhusu Manabii?

5. ․․․․․

Ni nabii gani aliyemtoroka Mfalme Yehoyakimu?

DOKEZO: Soma Yeremia 26:17-23.

6. ․․․․․

Hezekia alipokuwa mfalme, ni nani aliyetabiri kwamba Yerusalemu lingekuwa “marundo ya mabomoko”?

DOKEZO: Soma Yeremia 26:18.

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Baada ya kusoma kuhusu manabii hao wawili, kwa nini hupaswi kuogopa kuzungumza kumhusu Mungu?

DOKEZO: Soma Methali 29:25.

▪ Majibu kwenye ukurasa wa 21

MAJIBU YA UKURASA WA 31

1. Simulizi hilo halimtaji bibi-arusi.

2. Mabikira watano waliingia kwenye karamu.

3. Mabikira watano walikuwa na taa na vyombo vya mafuta huku wengine watano walikuwa na taa peke yake.

4. Kunapaswa kuwa na mlango ambao bwana-arusi anafunga.

5. Uria.—Yeremia 26:20.

6. Mika.