Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mizunguko Inayotegemeza Uhai

Mizunguko Inayotegemeza Uhai

Mizunguko Inayotegemeza Uhai

IKIWA mifumo ya kuingiza hewa safi na kuleta maji katika jiji fulani ingekatizwa, nayo mifumo ya kuondoa maji-taka izibwe, hilo lingesababisha magonjwa na kifo. Hata hivyo, sayari yetu haihitaji hewa safi na maji kutoka kwa sayari nyingine wala haihitaji kupeleka takataka kwenye sayari nyingine! Basi ni nini kinachowezesha dunia iwe mahali safi na salama pa kuishi? Jibu ni: mizunguko ya asili, kama vile mizunguko ya maji, kaboni, oksijeni, na nitrojeni, ambayo imeelezewa na kurahisishwa hapa kwa njia rahisi.

Mzunguko wa maji unatia ndani hatua tatu. 1. Nishati ya jua huvukiza maji na kuyainua kwenye angahewa. 2. Maji hayo safi hugandamana na kutokeza mawingu. 3. Nayo mawingu hutokeza mvua, mvua ya mawe, au theluji, ambayo hunyesha, na hivyo kukamilisha mzunguko huo. Lakini ni kiasi gani cha maji husafishwa na kutumiwa tena kila mwaka? Kulingana na makadirio, ni kiasi cha kutosha kufunika dunia yote kwa kina cha sentimita 100 hivi.

2

← ◯

3

1

↓ ↑

→ →

Mzunguko wa kaboni na oksijeni unahusisha hatua mbili kuu—usanidimwanga na kupumua. * Usanidimwanga hutumia mwangaza wa jua, kaboni dioksidi, na maji ili kutokeza wanga na oksijeni. Wanyama na wanadamu wanapopumua, hewa hiyo huchanganyika na wanga na oksijeni na kutokeza nishati, kaboni dioksidi, na maji. Kwa hiyo, kile kinachotokezwa na mfumo mmoja hutumiwa na mfumo ule mwingine, na hilo hutendeka taratibu bila kutokeza takataka wala kelele yoyote.

Oksijeni

← ←

↓ ↑

↓ ↑

↓ ↑

→ →

Kaboni dioksidi

Mzunguko wa nitrojeni ni muhimu ili kutokeza amino asidi, protini, na molekuli za vitu vingine vilivyooza. A. Mzunguko huo huanza wakati radi na bakteria zinapobadili nitrojeni iliyo hewani kuwa mchanganyiko unaoweza kufyonzwa na mimea. B. Nayo mimea hutumia mchanganyiko huo kutokeza molekuli za vitu vilivyooza. Wanyama hula mimea na hivyo wao pia wanapata nitrojeni. C. Mimea na wanyama wanapokufa, jamii nyingine za bakteria humeng’enya mchanganyiko huo wenye nitrojeni na hivyo kurudisha nitrojeni kwenye udongo na hewani.

← ← ← ← ← ← ← ← ← ←

↓ ↑

↓ Angahewa lina ↑

↓ asilimia 78 ya nitrojeni ↑

↓ ↑

↓ ↓ Molekuli za ↑

A ↓ vitu vilivyooza ↑

↓ Bakteria ↓ B ↑ ↓ C

→ Mchanganyiko wa nitrojeni Bakteria →

→ → →

Kusafisha na Kutumia Tena Takataka!

Fikiria hili: Kila mwaka, tekinolojia ya wanadamu imetokeza tani nyingi sana za takataka zenye sumu zisizoweza kutumiwa tena. Ingawa hivyo, dunia inasafisha na kutumia tena takataka zake zote kupitia mbinu za hali ya juu. “Nasibu peke yake haingeweza kutokeza” upatano huo wa kimazingira, anasema mwandishi wa mambo ya kidini na kisayansi M. A. Corey.

Ikimpa sifa yule anayestahili, Biblia inasema hivi: “Jinsi kazi zako zilivyo nyingi, Ee Yehova! Zote umezifanya kwa hekima.” (Zaburi 104:24) Wanadamu wameona hekima hiyo kwa njia ya pekee.

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 11 Huenda kemikali zilezile zikatumika katika mizunguko mbalimbali. Kwa mfano, kaboni dioksidi, wanga, na maji zina oksijeni. Kwa hiyo, oksijeni inatumika katika mzunguko wa kaboni na ule wa maji.