Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?

Soma Matendo 3:1-10. Kisha utazame picha. Kuna kasoro gani? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Kwa nini mitume walikuwa na uwezo wa kufanya miujiza? Hilo linatupa tumaini gani la wakati ujao?

DOKEZO: Soma Ufunuo 21:3, 4; 22:2.

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Katika Toleo Hili

Jibu maswali haya na utaje mistari ya Biblia ambayo haijaonyeshwa.

UKURASA WA 5 Ni nini kitatokea mvulana au msichana akifundishwa namna ya kuishi tangu utotoni? Methali 22:________

UKURASA WA 5 Mungu alifanya nini kutoka kwa mtu mmoja? Matendo 17:________

UKURASA WA 11 Maneno mema yatafanya nini? Methali 12:________

UKURASA WA 23 Ni nani aliye mkuu zaidi kati ya Wakristo? Luka 9:________

Unajua Nini Kuhusu Mwamuzi Ehudi?

Soma Waamuzi 3:12-30. Sasa jibu maswali yafuatayo.

4. ․․․․․

Alitoka kabila gani?

5. ․․․․․

Alikomboa Israeli kutoka kwa mtawala gani?

6. ․․․․․

Kweli au si kweli? Aliishi kabla ya Mfalme Daudi.

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Soma Waamuzi 3:15, 28. Kwa nini Yehova alimweka rasmi Ehudi? Ehudi alimsifu nani kwa sababu ya ushindi wake? Ukipata vipingamizi, unapaswa kufanya nini, na kwa nini?

▪ Majibu kwenye ukurasa wa 29

MAJIBU YA UKURASA WA 31

1. Petro na Yohana walikuwapo.

2. Mwanamume huyo alikuwa kilema, si kipofu.

3. Mwanamume kilema alikuwa karibu na lango la hekalu si mashambani.

4. Benyamini.—Waamuzi 3:15.

5. Egloni.—Waamuzi 3:14.

6. Kweli.