Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ramani ya Elektroniki

Ramani ya Elektroniki

Ramani ya Elektroniki

BILA shaka inaweza kuwa vigumu kwako kujua unakoelekea ukiwa katika mji usioufahamu. Kwa hiyo, baharia atajuaje anakoelekea kwa kuwa baharini hakuna alama zozote za kumwongoza? Kuwa tu na dira hakuwezi kumsaidia isipokuwa awe anajua mahali alipo na anapoelekea. Katika miaka ya 1730, mabaharia walianza kutambua mahali hususa walipo na kuamua ni njia gani watakayofuata kwenye ramani, baada ya kubuniwa kwa chombo kinachopima umbali wa jua au nyota kutoka kwenye upeo wa macho (sextant) na kifaa kinachosaidia kutambua mahali meli ilipo baharini. Lakini walitumia saa nyingi kupiga hesabu hiyo.

Leo madereva katika nchi nyingi hutumia vifaa visivyogharimu sana vilivyounganishwa na Mfumo wa Kupokea Habari Kutoka kwa Setilaiti (GPS). Unachohitaji kufanya ni kuingiza habari kuhusu mahali unapoelekea. Kifaa hicho kinaweza kukuonyesha mahali hususa unapotaka kwenda. Kisha kitakuelekeza huko. Mfumo huo unafanya kazi kwa njia gani?

Vifaa hivyo hutegemea setilaiti 30 hivi. Kila setilaiti hutuma habari ikionyesha mahali ilipo na kuonyesha saa kwa muda mfupi usiozidi sekunde moja. Mara tu kifaa chako kinapounganishwa na setilaiti kadhaa, kinapima kwa usahihi muda ambao habari hiyo inachukua kutoka kwenye setilaiti hadi kwenye kifaa chako. Kinapofanya hivyo, kinatambua mahali ulipo. Je, unaweza kuwazia jinsi hesabu hiyo ilivyo tata? Katika muda wa sekunde chache tu, kinapima umbali kati ya setilaiti tatu, zote zikiwa mbali sana na zikielekea upande tofauti kwa mwendo wa kasi sana.

Maprofesa Bradford Parkinson na Ivan Getting walibuni mfumo huo wa setilaiti mwanzoni mwa miaka ya 1960. Ingawa mwanzoni mfumo huo ulibuniwa ili utumiwe na jeshi, baadaye ulianza kutumiwa na kila mtu kufikia mwaka wa 1996. Kifaa cha kupokea habari kutoka kwenye setilaiti ni uthibitisho mkubwa wa maendeleo ya tekinolojia ya kompyuta, lakini je, hiyo ndiyo tekinolojia ya kwanza ya aina yake?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 8]

Globe: Based on NASA photo