Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Usingizi—Kwa Nini Ni Muhimu Sana?

Usingizi—Kwa Nini Ni Muhimu Sana?

Usingizi—Kwa Nini Ni Muhimu Sana?

● Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kwamba kwa wastani, watu wa Amerika Kaskazini hulala kati ya saa saba na saa saba na nusu kila siku. * Usingizi ni muhimu kadiri gani? Mtu hupitia hatua kadhaa za usingizi ambazo zinajulikana kama vipindi vya kusogeza macho haraka kwa kila dakika 60 hadi 90 anapokuwa amelala. Wakati huo ndipo ubongo hufanya kazi sana na watafiti wanaamini kwamba unafanya kazi ya kujirekebisha. Wataalamu fulani wanasema kwamba athari za kudumu husababishwa mwilini kipindi hicho kinapokatizwa na usingizi kutoweka. Utendaji wa ubongo huathiriwa na hilo humzuia mtu asitimize mengi na apatwe na magonjwa mengi.

Vitu fulani kama vile kafeini, vinaweza kuzuia kwa muda fulani kemikali zinazousaidia mwili kutambua kwamba mtu anahitaji kulala. Hata hivyo, ubongo wetu una uwezo wa kufanya tusinzie kidogo ikiwa hatukupata usingizi wa kutosha. Kulingana na gazeti The Toronto Star, “hata iwe unafanya nini, mara kwa mara ubongo wako wenye deni la usingizi utashikwa na usingizi na kuingia kwenye hatua ya kwanza ya usingizi kwa muda wa kati ya sekunde kumi na dakika moja hivi.” Hebu wazia ukiendesha gari kwa mwendo wa kilomita 48 kwa saa na usinzie kwa sekunde kumi. Wakati huo, utakuwa umesafiri umbali ulio sawa na uwanja wa mpira. Isitoshe, kukosa usingizi wa kutosha kunaweza kudhoofisha mfumo wako wa kinga, kwa sababu chembe za T ambazo husaidia kupigana na virusi, hutokezwa wakati umelala. Pia tunapolala mwili wetu hutokeza homoni inayoitwa leptin ambayo husaidia kusawazisha hamu ya kula. Kwa kweli, mwili wetu unahitaji usingizi kama vile tu unavyohitaji mazoezi na lishe bora.

Je, kufanya kazi ya ziada kunafanya usipate usingizi wa kutosha? Au je, una mahangaiko ya maisha na wasiwasi mwingi kuhusu mali ulizokusanya kwa ajili ya wakati ujao? Mfalme Sulemani mwenye hekima alisema hivi pindi moja: “Usingizi wa mtumishi ni mtamu, bila kujali kama anakula kidogo au kingi; lakini wingi alio nao tajiri haumruhusu kulala.”—Mhubiri 5:12.

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 2 Ona habari yenye kichwa “Je, Una Deni la Usingizi?” katika Amkeni! la Februari 8, 2004 (8/2/2004).