Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Kuna Tofauti Gani?

Je, unaweza kutambua tofauti tatu kati ya picha A na picha B? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapo chini, na ukamilishe picha hizo kwa kuzipaka rangi.

DOKEZO: Soma Kutoka 28:9-12, 33, 36, 37.

1 ․․․․․

2 ․․․․․

3 ․․․․․

4. Ni picha gani sahihi, iliyo upande wa kulia au kushoto?

․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Neno “takatifu” linamaanisha nini? Kwa nini ni muhimu kwa waabudu wa Yehova kuwa watakatifu? Unaweza kuonyesha kwa njia gani kwamba unajaribu kuwa mtakatifu?

DOKEZO: Soma 2 Wakorintho 7:1.

UTENDAJI WA FAMILIA:

Kila mtu katika familia afanye utafiti kuhusu jukumu la kuhani mkuu wa Israeli. Kisha mkutane na kueleza mambo mliyojifunza. Kwa mfano, kuhani mkuu alikuwa na madaraka gani?

DOKEZO: Soma Mambo ya Walawi 9:7; Kumbukumbu la Torati 17:9-11.

Ni katika njia gani Yesu Kristo anathibitika kuwa Kuhani Mkuu bora zaidi?

DOKEZO: Soma Waebrania 4:14-16; 7:26-28; 9:11-14.

Kusanya na Ujifunze

Kata, kunja katikati, na uhifadhi

KADI YA BIBLIA 3 RUTHU

MASWALI

A. Kamilisha maneno ambayo Ruthu alimwambia Naomi: “Watu wako watakuwa . . .”

B. Ni katika njia gani Ruthu ni mfano mzuri kwa watu wanaowatunza wagonjwa na wazee?

C. Jaza mapengo. Ruthu aliolewa na ․․․․․ naye akawa nyanya ya ․․․․․ na ․․․․․ .

[Chati]

4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.

Adamu aumbwa Aliishi miaka Kitabu cha mwisho

ya 1200 K.W.K. cha Biblia kinaandikwa

[Ramani]

Alihama kutoka Moabu hadi Bethlehemu

MOABU

Bethlehemu

RUTHU

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Mjane mwaminifu wa Moabu ambaye alimtegemeza mama-mkwe wake, Naomi. Upendo mshikamanifu wa Ruthu kumwelekea Naomi na bidii yake ya kumtumikia Yehova ilimpa nguvu za kuondoka nchi aliyozaliwa na kuhamia Bethlehemu. Watu walimwambia Naomi, “Binti-mkwe wako . . . ni bora kwako kuliko wana saba.”—Ruthu 4:14, 15.

MAJIBU

A. “. . . watu wangu, na Mungu wako Mungu wangu.”—Ruthu 1:16.

B. Ruthu alikuwa na roho ya kujidhabihu na bidii.—Ruthu 2:7, 10-12, 17; 3:11.

C. Boazi, Mfalme Daudi, Yesu Kristo.—Mathayo 1:5, 6, 16.

Watu na Nchi

5. Jina langu ni Shaé. Ninaishi nchini Uingereza, karibu na bara la Ulaya. Ni Mashahidi wangapi wa Yehova wanaoishi nchini Uingereza? Je, ni 13,300, 133,000, au 333,000?

6. Ni alama gani inayoonyesha eneo ninaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, na uchore alama nyingine katika eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Uingereza.

A

B

C

D

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

● Majibu ya ukurasa wa 30 na 31 kwenye ukurasa wa 7

MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31

1. Maneno juu ya kilemba.

2. Mawe ya shohamu juu ya mabega.

3. Kengele kwenye upindo.

4. Ile ya upande wa kushoto.

5. 133,000.

6. B.