Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Yai la Ndege

Yai la Ndege

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Yai la Ndege

● Yai la ndege limesemwa kuwa ni “muujiza wa upakizi.” Kwa nini?

Fikiria hili: Ingawa linaonekana gumu, kaka la yai lililo na kalisi nyingi lina mashimo 8,000 madogo sana. Mashimo hayo huruhusu oksijeni iingie na kaboni-dioksidi itoke—mzunguko muhimu ambao unasaidia kiini-tete kupumua. Hata hivyo, kaka hilo na tando kadhaa huzuia bakteria zisiathiri kiini-tete hicho. Albumini—ambayo ni jelatini fulani iliyo na maji mengi—husaidia yai lisitikisike sana.

Watafiti wangependa kuiga muundo wa yai ili kutokeza bidhaa za upakizi zinazoweza kusaidia matunda kuhimili mshtuko na kuyalinda yasiathiriwe na bakteria na vijidudu. Hata hivyo, “si rahisi kuiga vitu vya asili,” anaandika Marianne Botta Diener katika gazeti Vivai. Anasema kwamba majaribio ambayo yamefanywa kufikia sasa yamedhuru mazingira.

Una maoni gani? Je, ‘muujiza huu wa upakizi,’ yaani, yai la ndege, ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

[Mchoro katika ukurasa wa 28]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

NDANI YA YAI

Kaka

Kiini

Chalaza (hushikilia kiini)

Utando wa nje

Utando wa ndani

Sehemu ambayo kiini-tete huanzia

Albumini nyepesi

Albumini nzito

Sehemu yenye hewa