Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Patanisha Picha na Maandishi

Soma Mhubiri 2:3-10. Chora mstari kuunganisha kila picha na mstari wa Biblia unaopatana nao. (Picha hazijapangwa kwa mpangilio unaofaa.) Kamilisha picha hizi kwa kuzipaka rangi.

1. Mstari wa 3

2. Mstari wa 4

3. Mstari wa 5

4. Mstari wa 6

5. Mstari wa 7

6. Mstari wa 8

A

B

C

D

E

F

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Je, Sulemani alifurahia mambo aliyotimiza kwa ajili yake mwenyewe?

DOKEZO: Soma Mhubiri 2:11.

Maneno “ubatili na kufuatilia upepo” yanamaanisha nini? Ni utendaji gani utakaokufanya uwe na furaha ya kweli?

DOKEZO: Soma Luka 6:38; Matendo 20:35.

UTENDAJI WA FAMILIA:

Soma Mhubiri 3:1-8. Mwombe kila mtu katika familia aandike utendaji mmoja ulioorodheshwa katika mistari hiyo kwenye karatasi tofauti. Tieni karatasi hizo katika boksi. Kila mmoja achukue karatasi moja na, bila kusema lolote, aigize utendaji ulioonyeshwa kwenye karatasi hiyo. Oneni ikiwa wengine katika familia wanaweza kutambua utendaji unaoigizwa.

Kusanya na Ujifunze

Kata, kunja katikati, na uhifadhi

KADI YA BIBLIA 11 YOSEFU

MASWALI

A. Jaza mapengo. Ndugu wa kambo wa Yosefu walimwita “yule ․․․․․,” na wakamwuza utumwani kwa vipande ․․․․․ vya fedha.

B. Aliposhinikizwa na mke wa Potifa wafanye ngono, Yosefu alijibu hivi kwa ujasiri, “Ninawezaje kufanya ubaya huu mkubwa na . . .”

C. Kwa nini Farao alimweka Yosefu kuwa mtawala wa pili wa Misri?

[Chati]

4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.

Adamu aumbwa Aliishi katika Kitabu cha

miaka ya mwisho cha

1700 K.W.K Biblia kinaandikwa

[Ramani]

Alichukuliwa kutoka Dothani hadi Misri

Dothani

MISRI

YOSEFU

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Mwana wa kwanza wa Yakobo na Raheli. (Mwanzo 35:24) Ndugu zake wa kambo wenye wivu walimwuza utumwani Misri ambako alikaa kwa miaka 13 hivi akiwa mtumwa na mfungwa. Badala ya kulipiza kisasi, Yosefu aliwasamehe ndugu zake wa kambo waliotubu. (Mwanzo 50:15-21) Ingawa alikuwa mbali na nyumbani, alimheshimu Yehova, akadumisha usafi wa maadili, akafanya kazi kwa bidii, na alikuwa mwenye kuaminika.—Mwanzo 39:1-23.

MAJIBU

A. Mwota-ndoto, 20.—Mwanzo 37:19, 28.

B. “. . . kwa kweli nimtendee Mungu dhambi?”—Mwanzo 39:9.

C. Alijua kwamba roho ya Mungu ilimfanya Yosefu kuwa mwenye hekima na busara.—Mwanzo 41:38-41.

Watu na Nchi

7. Jina langu ni Anietie. Nina umri wa miaka saba, na ninaishi nchini Nigeria. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Nigeria? Ni 190,000, 290,000, au 390,000?

8. Ni alama gani inayoonyesha eneo ninaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, na uchore alama nyingine kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Nigeria.

A

B

C

D

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Ili uchapishe nakala za ziada za “Mazungumzo ya Familia,” nenda kwenye www.pr418.com

● Majibu ya “MAZUNGUMZO YA FAMILIA” kwenye ukurasa wa 15

MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31

1. 1 inapatana na F.

2. 2 inapatana na E.

3. 3 inapatana na A.

4. 4 inapatana na C.

5. 5 inapatana na B.

6. 6 inapatana na D.

7. 290,000.

8. C.