Ukosefu wa Unyoofu Umeenea Sana!
Ukosefu wa Unyoofu Umeenea Sana!
Danny * anafanya kazi katika kampuni moja kubwa nchini Hong Kong. Alipokuwa akitembelea kiwanda fulani, alieleza wasiwasi wake kwamba kiwanda hicho hakingeweza kutimiza viwango vinavyohitajiwa ili kutokeza bidhaa za kampuni yao. Baadaye walipokuwa wakila, meneja wa kiwanda hicho alimpa Danny bahasha fulani. Ndani kulikuwa na rushwa ya maelfu ya dola—kiasi cha dola hizo kilikuwa sawa na mshahara wake wa mwaka mzima.
● Kisa cha Danny si cha kipekee. Ulimwenguni pote, ukosefu wa unyoofu umeenea sana. Kwa mfano, hati za mahakamani zinaonyesha kwamba kati ya mwaka wa 2001 na 2007, kiwanda kimoja kikubwa nchini Ujerumani kilitoa rushwa ya jumla ya dola bilioni 1.4 ili kipate kandarasi mbalimbali.
Ingawa kashfa za karibuni zinazohusisha makampuni makubwa zimefanya kuwe na mabadiliko fulani, hali kwa ujumla inaendelea kuzorota. Uchunguzi uliofanywa mwaka wa 2010 na shirika la Transparency International ulionyesha kwamba ulimwenguni pote, “viwango vya ufisadi vimeongezeka katika miaka mitatu iliyopita.”
Kwa nini kuna ukosefu mwingi wa unyoofu? Je, kuna faida zozote za kuwa mnyoofu? Ikiwa kuna faida, mtu anawezaje kuwa mnyoofu? Je, Biblia inaweza kutusaidia?
[Maelezo ya Chini]
^ fu. 2 Baadhi ya majina katika mfululizo huu yamebadilishwa.