Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Vijana Huuliza

Je, Ni Vibaya Kuwa Maarufu?

Je, Ni Vibaya Kuwa Maarufu?

Andika maneno yatakayokamilisha sentensi ifuatayo:

Ni vizuri ․․․․․ kuwa maarufu.

  1. A. nyakati zote

  2. B. nyakati fulani

  3. C. usiwahi kamwe

JIBU sahihi ni “B.” Kwa nini? Kwa sababu kuwa maarufu humaanisha kwamba unapendwa na watu wengi—na hilo si jambo baya! Biblia ilitabiri kwamba Wakristo wangekuwa “nuru ya mataifa” na kwamba watu wangevutwa kwao. (Isaya 42:6; Matendo 13:47) Kwa njia hiyo, inaweza kusemwa kuwa Wakristo ni watu maarufu.

Je, wajua?

Yesu alikuwa maarufu. Hata alipokuwa kijana, alipata “kibali kwa Mungu na wanadamu.” (Luka 2:52) Na Biblia inasema kwamba Yesu alipokuwa mtu mzima, “umati mkubwa ukamfuata kutoka Galilaya na Dekapoli na Yerusalemu na Yudea na kutoka upande ule mwingine wa Yordani.”—Mathayo 4:25.

Kwa nini jambo hilo lilifaa?

Kwa sababu Yesu hakutaka utukufu au kujitafutia umaarufu, na hakuwa akiomba-omba kibali cha watu wengine. Yesu alifanya alichopaswa kufanya—jambo ambalo nyakati nyingine lilimfanya awe maarufu. (Yohana 8:29, 30) Wakati huohuo, Yesu alitambua kwamba, kibali alichopata kutoka kwa watu ambao hawakuwa na msimamo kilikuwa cha muda mfupi tu. Alisema wazi kwamba baadaye watu wangemuua!—Luka 9: 22.

Jambo Muhimu:

Umaarufu ni kama utajiri. Si mara zote kuwa tajiri ni vibaya. Tatizo ni jinsi watu wanavyong’ang’ana kuupata—au kuudumisha.

Tahadhari!

Vijana wengi hufanya juu chini ili wawe maarufu. Wengine wako tayari kufanya chochote ambacho watu wengi wanawashinikiza kufanya mradi tu wawe maarufu. Wengine ni waonevu wanaowalazimisha wengine wapendezwe nao—hata kama ni kwa sababu tu wanawaogopa. *

Katika kurasa zinazofuata, tutazungumzia njia hizo mbili mbaya za kujipatia umaarufu. Halafu tutachunguza njia bora ya kufanya hivyo.

 

^ fu. 12 Biblia inawataja waonevu walioitwa “Wanefili,” ambao pia wanajulikana kama “wanaume wenye sifa.” Lengo lao kuu lilikuwa kujitafutia utukufu wao wenyewe.—Mwanzo 6:4.