Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Kuna Tofauti Gani?

Je, unaweza kutambua tofauti tatu kati ya picha A na picha B? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapo chini, na ukamilishe picha hizo kwa kuzipaka rangi.

DOKEZO: Soma 1 Samweli 16:1-3, 6-13.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

4. Ni picha gani iliyo sahihi, picha A au picha B?

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Yehova huona nini anapomtazama mtu? Biblia inamaanisha nini inaposema ‘Yehova, huuona moyo’?

DOKEZO: Soma Yeremia 17:10.

Sura ya nje ya mtu ina thamani gani kwa Yehova?

DOKEZO: Soma Methali 11:22; 31:30; 1 Petro 3:3, 4.

Ni sifa gani zitakazofanya upendeze machoni pa Mungu?

DOKEZO: Soma Luka 10:27; 2 Petro 1:5-8.

UTENDAJI WA FAMILIA:

Soma Wagalatia 5:22, 23. Andika kila moja ya zile sifa tisa kwenye karatasi tofauti. Chagueni mtu mmoja wa familia, na kwa kutumia gundi, mbandike kikaratasi kimoja mgongoni mwake. Msimruhusu aone ni sifa gani mliyombandika. Acheni ajaribu kutambua sifa hiyo kwa kuwauliza maswali kuihusu. Washiriki wengine wa familia watoe majibu ya ndiyo au la peke yake kwa maswali anayouliza.

Kusanya na Ujifunze

Kata, kunja katikati, na uhifadhi

KADI YA BIBLIA 15 DAUDI

MASWALI

A. Daudi na Yesu walizaliwa katika mji upi?

B. Alipokuwa mvulana, Daudi alikuwa ․․․․․ ambaye kwa ujasiri aliua ․․․․․ na ․․․․․

C. Kamilisha maneno ya Daudi: “Nawe, Sulemani mwanangu, mjue . . . ”

[Chati]

4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.

Adamu aumbwa Aliishi katika Kitabu cha

miaka ya mwisho cha

1000 K.W.K. Biblia kinaandikwa

[Ramani]

Alihama kutoka Bethlehemu hadi Yerusalemu

Yerusalemu

Bethlehemu

Alipigana na Goliathi kwenye nchi tambarare ya chini ya Ela.​—1 Samweli 17:2

Nchi tambarare ya chini ya Ela

DAUDI

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Mwana wa Yese, na Mfalme wa pili wa Israeli. Mshairi stadi na mwanamuziki, Daudi aliandika zaidi ya zaburi 73. Alitafuta mwongozo wa Yehova kwa unyenyekevu katika maisha yake. (1 Samweli 23:2; 30:8; 2 Samweli 2:1) Yehova alimwita Daudi “mtu anayekubalika kwa moyo wangu.”—Matendo 13:22.

MAJIBU

A. Bethlehemu (ya Yudea).—Yohana 7:42.

B. mchungaji, simba, dubu.—1 Samweli 17:34, 35; Zaburi 78:70, 71.

C. “. . . Mungu wa baba yako, umtumikie kwa moyo kamili.”—1 Mambo ya Nyakati 28:9.

Watu na Nchi

5. Jina langu ni Olivia. Nina umri wa miaka sita, ninaishi nchini Indonesia. Ni Mashahidi wangapi wa Yehova wanaoishi nchini Indonesia? Je, ni 22,300, 42,800, au 63,900?

6. Ni alama gani inayoonyesha eneo ninaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, na uchore alama nyingine katika eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Indonesia.

A

B

C

D

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Ili uchapishe nakala zaidi za “Mazungumzo ya Familia,” nenda kwenye www.pr418.com

● Majibu ya “MAZUNGUMZO YA FAMILIA” kwenye ukurasa wa 22

MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31

1. Picha moja ina mbuzi na nyingine ina ng’ombe.

2. Picha moja ina binti na ile nyingine hayuko.

3. Picha moja ina kiriba na ile nyingine inaonyesha pembe iliyojazwa mafuta.

4. B.

5. 22,300.

6. D.