Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Ni Nini Kimekosekana Katika Picha Hii?

Soma 1 Mambo ya Nyakati 16:1, 2, 4-10. Sasa itazame picha. Ni vitu gani vimekosekana? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini. Unganisha nukta zilizopo ili ukamilishe picha hii, kisha uipake rangi.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

[Mchoro]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Je, Yehova Mungu hufurahi tunapotumia muziki na tunapoimba katika ibada yetu? Kwa nini unajibu hivyo?

DOKEZO: Soma 2 Mambo ya Nyakati 5:13, 14; Waefeso 5:19.

Je, unaweza kutaja masimulizi mengine katika Biblia ambapo nyimbo zilitumiwa katika ibada ya kweli?

DOKEZO: Soma Kutoka 15:1-20; Marko 14:26; Matendo 16:25.

Ni mtazamo gani unaoweza kukusaidia kumwimbia Yehova hata kama una haya au unahisi kwamba wengine wanaimba vizuri zaidi kuliko wewe?

DOKEZO: Soma Zaburi 33:1-3.

UTENDAJI WA FAMILIA:

Mwombe kila mmoja katika familia achague wimbo anaoupenda wa kumsifu Yehova. Mkiwa familia, fanyeni mazoezi ya kuimba nyimbo hizo hadi mzifahamu vizuri.

Kusanya na Ujifunze

Kata, kunja katikati, na uhifadhi

KADI YA BIBLIA 17 YONA

MASWALI

A. Yona alitumwa kwenda kuhubiri ․․․․․, ambako watu zaidi ya ․․․․․ waliishi.

B. Ingawa mwanzoni Yona alitoroka mgawo wake, alifanya jambo gani la ujasiri ili kuwaokoa wengine?

C. Kamilisha maneno haya ya Biblia: “Yona akawa katika tumbo  . . .”

[Chati]

4026 K.W.K. Adamu aumbwa

Aliishi miaka ya 840 K.W.K.

1 W.K.

98 W.K. Kitabu cha mwisho cha Biblia chaandikwa

[Ramani]

Alitoroka kutoka Gath-heferi hadi Tarshishi

Gath-heferi

TARSHISHI

Ninawi

YONA

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Nabii wa Yehova aliyetumika wakati Mfalme Yeroboamu wa Pili alipokuwa akitawala. (2 Wafalme 14:23-25) Yehova alimfundisha Yona kujali mahitaji ya wengine, si kujielekezea fikira mwenyewe. (Yona 4:6-11) Mambo yaliyompata Yona yanatufundisha kwamba Yehova ni mwenye subira sana, ni mwenye rehema, na mwenye fadhili kuelekea wanadamu watenda dhambi.

MAJIBU

A. Ninawi, 120,000.—Yona 1:1, 2; 4:11.

B. Aliwaambia mabaharia wamtupe baharini ili bahari itulie.—Yona 1:3, 9-16.

C. “ . . . la samaki huyo siku tatu mchana na usiku.”—Yona 1:17.

Watu na Nchi

4. Majina yetu ni Melissa na Edilo. Nina umri wa miaka 9 na Edilo ana umri wa miaka 7. Tunaishi Kuba. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Kuba? Ni 51,000, 91,000, au 131,000?

5. Ni alama gani inayoonyesha eneo tunaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, na uchore alama nyingine kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Kuba.

A

B

C

D

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Ili uchapishe nakala za ziada za “Mazungumzo ya Familia,” nenda kwenye www.pr418.com

● Majibu ya “MAZUNGUMZO YA FAMILIA” kwenye ukurasa wa 14

MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31

1. Hema linalofunika Sanduku.

2. Kinubi.

3. Tarumbeta.

4. 91,000.

5. C.