Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kombe la Konokono Anayeitwa Clusterwink

Kombe la Konokono Anayeitwa Clusterwink

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Kombe la Konokono Anayeitwa Clusterwink

● Viumbe wengi wa baharini wana uwezo wa kutokeza mwanga. Konokono anayeitwa Clusterwink hutumia uwezo huo kwa njia ya pekee. Anaponyemelewa na kaa, konokono huyo huingia ndani ya kombe lake na kutokeza mimweko inayomtisha kaa huyo. Lakini mwanga huo unawezaje kupenya kombe la konokono huyo?

Fikiria hili: Badala ya kuzuia mwanga, kombe la konokono huyo huutawanya mwanga huo. Dimitri Deheyn na Nerida Wilson, wanasayansi katika Taasisi ya Sayansi ya Bahari ya Scripps huko San Diego, California, Marekani, waligundua kwamba mwanga unaotokezwa na konokono huyo unaenezwa katika kombe lote kwa kiasi kinacholingana, kisha kombe hilo hutawanya mwanga mara kumi zaidi ya kifaa chochote kilichotengenezwa viwandani kilicho na unene kama wa kombe hilo (0.5 mm). Wakati huohuo, uwezo wa kombe hilo kuangaza mwanga huo ni mara nane zaidi ya vifaa vingine vilivyotengenezwa na wanadamu. Kwa kushangaza, makombe ya konokono wengine wa jamii hiyo hayana uwezo huo wa pekee wa kutawanya na kuangaza mwanga. Hilo halishangazi kwa kuwa rangi ya mwanga unaotokezwa na konokono huyo ndiyo husambaa mbali zaidi katika maji ya bahari.

Dakt. Deheyn anasema kwamba kujifunza kuhusu konokono huyo “kunaweza kuwa muhimu katika kutokeza vifaa vinavyoweza kusambaza mwangaza kwa njia nzuri zaidi.” Uchunguzi huo utafaidi sana taaluma ya biophotonics ambayo hutumia nuru kwa ajili ya uchunguzi wa kitiba na matibabu. Katika kipindi hiki ambapo watu wengi wanatumia balbu, iwapo vifaa vinavyoweza kutawanya kiasi kidogo sana cha nuru vitabuniwa, basi hilo litasaidia sana kuokoa nishati.

Una maoni gani? Je, kombe la konokono anayeitwa clusterwink lilitokezwa na mageuzi? Au lilibuniwa?

[Picha katika ukurasa wa 18]

Kombe la konokono likiwa chini ya nuru ya kawaida

[Picha katika ukurasa wa 18]

Kombe la konokono linapotawanya nuru

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 18]

Left: www.robastra.com; center and right: Courtesy of Dr. D. Deheyn, Scripps Institution of Oceanography, UC San Diego