Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

“Simu za mkononi zinaweza kumfanya mtu asisumbuliwe na watu wanaotaka kuongea naye ana kwa ana—asilimia 13 ya watu wenye simu za mkononi wamejifanya kuwa wanaongea na mtu fulani kwenye simu zao ili wasisumbuliwe na mtu aliye karibu nao.”—KITUO CHA UTAFITI CHA PEW, MAREKANI.

Kwa miaka mitano sasa, kiasi cha barafu inayofunika bahari huko Aktiki kimepungua sana wakati wa majira ya kiangazi.—SHIRIKA LA HABARI LA BBC, UINGEREZA.

“Karibu asilimia 47 ya mashamba barani Afrika hayalimwi.”—THE WITNESS, AFRIKA KUSINI.

“Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, nchi 10 (Uholanzi, Ubelgiji, Kanada, Hispania, Afrika Kusini, Norway, Sweden, Ureno, Iceland, na Argentina) zimehalalisha ndoa za watu wa jinsia moja.” —FAMILY RELATIONS, MAREKANI.

Mizozo Imeacha Athari za Kudumu

Utafiti uliofanywa huko Ireland Kaskazini unaonyesha kwamba mizozo ya kidini na ya kisiasa imeacha athari za kudumu. Mizozo hiyo iliendelea kwa kipindi cha miaka 30 hivi na ilisababisha asilimia 66 ya wakazi wa nchi hiyo wapatwe na matukio yenye kutisha. Kituo cha Bamford cha Afya ya Akili na Hali Njema katika Chuo Kikuu cha Ulster kiligundua kwamba angalau mtu 1 kati ya 10 wanaoishi Ireland Kaskazini ataugua ugonjwa wa mfadhaiko unaosababishwa na tukio lenye kutisha—“moja kati ya viwango vya juu zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine zote,” linasema gazeti The Irish Times. Gazeti hilo linaendelea kusema kwamba mizozo hiyo “ilikuwa miongoni mwa migogoro mibaya zaidi ulimwenguni, iliyosababisha kifo cha mtu mmoja kati ya 500 [nchini humo].”

Hali Mbaya ya Hewa Ni “Jambo la Kawaida”

Hali ya hewa nchini Marekani inazidi kubadilika-badilika. Hali ambayo zamani ilisemekana kuwa mbaya sana, yaani, mafuriko makubwa, ukame mbaya sana, na dhoruba za theluji zinazotisha, siku hizi ni “jambo la kawaida.” Kwenye kongamano lililopangwa na Chama cha Wanasayansi Wanaojali, Katharine Hayhoe, mtaalamu wa hali ya hewa wa Chuo Kikuu cha Tech huko Texas, aliwaambia wenzake hivi: “Tumezoea hali fulani za hewa lakini sasa kuna mambo mengi yanayofanyika ambayo si ya kawaida.” Hayhoe na wataalamu wengine wanaamini kwamba utendaji wa wanadamu ndio unaosababisha mabadiliko ya hali ya hewa na bado tunatarajia hali mbaya sana ya hewa.