Je, Ni Kazi Ya Ubuni?
Vipokezi vya Mbawakawa Anayeitwa Black Fire
Kwa nini? Kwa sababu, miti iliyotoka tu kuchomeka ni mahali panapofaa sana kwa wadudu hao kutaga mayai yao. Isitoshe, moto hufukuza wanyama wawindaji, na hilo huwapa mbawakawa hao nafasi ya kula, kujamiiana, na kutaga mayai yao bila wasiwasi. Lakini mbawakawa hao hutambuaje mahali palipo na moto msituni?
Fikiria hili: Kando ya miguu yao ya katikati, mbawakawa hao wana matundu yaliyo kati ya mianzi ya pua na macho ambayo yanaweza kutambua mnururisho kutoka kwenye moto wa msitu. Mnururisho huo hufanya vipokezi hivyo viwe na joto na hivyo kumfanya mbawakawa aelekee mahali ambapo moto upo.
Mbali na hilo, mbawakawa hao wana vipokezi vingine vinavyowasaidia kutambua mahali moto ulipo. Moto unapoteketeza miti wanayoipenda sana, antena za mbawakawa hao hutambua kiasi kidogo sana cha kemikali fulani ambazo moto huo hutokeza. Kulingana na watafiti fulani, mbawakawa hao wana uwezo wa kutumia antena zao kutambua mahali ambapo mti mmoja unaochomeka upo hata ukiwa umbali wa kilomita moja hivi. Wanapotumia uwezo wao mbalimbali, inaonekana kwamba mbawakawa hao wanaweza kutambua na kupata mioto ya msituni wakiwa umbali wa kilomita 48.3!
Watafiti wanachunguza antena za mbawakawa huyo anayeitwa black fire pamoja na matundu yake yanayomsaidia kutambua mnururisho ili waboreshe vifaa vinavyotumiwa kutambua miale ya infrared na moto. Kwa kuwa vipokezi vya kawaida vinavyotumiwa kutambua miale ya infrared hupata joto sana na lazima vipozwe, mbawakawa huyo anaweza kuwasaidia wanasayansi kutokeza vipokezi bora ambavyo joto lake halipandi sana. Antena za mbawakawa huyo zimewachochea mainjinia kutokeza mifumo ya hali ya juu ya kutambua moto ambayo inaweza kutofautisha kati ya kemikali zinazotokezwa na mioto na kemikali nyingine zilizo hewani.
Watafiti wameshangazwa na uwezo wa ajabu ambao mbawakawa huyo hutumia kupata mahali pa kutaga mayai yake. “Mbawakawa hao walipataje uwezo huo wa kutambua mahali pa kutagia mayai?” akauliza E. Richard Hoebeke, mtaalamu wa mbawakawa katika Chuo Kikuu cha Cornell, huko Marekani. “Hebu fikiria jinsi tunavyojua machache sana kuhusu wadudu walio na mifumo ya kuhisi ya hali ya juu na iliyo tata.”
Una maoni gani? Je, uwezo wa mbawakawa anayeitwa black fire wa kutambua mahali palipo na moto msituni ulitokea kupitia mageuzi? Au ulibuniwa?