Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

 NCHI NA WATU

Kutembelea Brazili

Kutembelea Brazili

Chakula kitamu cha kienyeji cha Wabrazili kinachoitwa feijoada

Toucan

WAKAZI wa awali wa Brazili walikuwa wawindaji na wakulima. Wavumbuzi Wareno walileta dini ya Katoliki nchini humo, na hatimaye makanisa mengi yakajengwa, na baadhi yake yalipambwa kwa michongo ya mbao iliyofunikwa kwa dhahabu.

Kuanzia katikati mwa karne ya 16 mpaka katikati mwa karne ya 19, meli ziliwasafirisha watumwa milioni nne hivi kutoka Afrika hadi Brazili ili wakafanye kazi katika mashamba. Waafrika hao walienda pamoja na desturi zao ambazo zilitokeza dini kama vile macumba na dhehebu la candomblé ambazo zina mchanganyiko wa imani za Kiafrika na Kibrazili. Uvutano wa Kiafrika unaonekana pia katika muziki, dansi na chakula cha Brazili.

Chakula cha wenyeji kinachoitwa feijoada kilichotokana na Wareno, ni mchuzi wa nyama na maharagwe meusi, na huliwa pamoja na wali na mboga za majani. Katika karne ya 19 na 20, mamilioni ya watu kutoka Japani, Ulaya (hasa kutoka Hispania, Italia,  Poland, na Ujerumani), na pia kutoka sehemu nyingine walihamia nchini Brazili.

Leo, kuna Mashahidi wa Yehova wapatao 750,000 katika makutaniko zaidi ya 11,000 kotekote nchini Brazili. Wanawafundisha Biblia watu zaidi ya 800,000. Ili Mashahidi wawe na majengo ya ibada, vikundi 31 vya ujenzi hushirikiana na Mashahidi wenyeji kujenga na kukarabati Majumba ya Ufalme 250 mpaka 300 hivi kila mwaka. Kuanzia Machi 2000 mpaka sasa, majengo ya ibada 3,647 yamekamilishwa.

JE, WAJUA?

Mto Amazoni humwaga maji mengi zaidi baharini kuliko mto mwingine wowote na una urefu wa zaidi ya kilomita 6,275

Bonde la Mto Amazoni lina msitu mkubwa zaidi wa mvua ulimwenguni