Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

MAREKANI

“Gazeti la New York Times liliripoti kwamba “mtu anayevuta sigara, alimgharimu mwajiri wake . . . dola 5,816 zaidi kila mwaka ikilinganishwa na mtu asiyevuta sigara.” Uchunguzi uliofanywa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Ohio, unaonyesha kwamba gharama hizo zilitokana na muda unaotumiwa kuvuta sigara kazini, gharama za juu za matibabu, na kutofika kazini. Jambo lingine ni kwamba ubora wa kazi uliathiriwa kwa sababu ya matokeo ya kuacha kuvuta sigara.

Italia

“Makasisi na wafuasi hawatendi kulingana na mambo wanayosema, na hilo linafanya watu wengi wakose imani na Kanisa.”—Papa Francis.

Malasia

MWenye mamlaka nchini Malasia walipata tani 24 za pembe za ndovu, yaani, zaidi ya pembe 1,000 zilizoingizwa nchini kiharamu zikiwa zimefichwa ndani ya shehena mbili zilizobeba mbao za mkangazi. Wahifadhi wa mazingira wamesema kwamba hicho ndicho kiwango kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa. Pembe hizo zilikuwa zikisafirishwa kutoka Togo kwenda China.

Afrika

Kulingana na ripoti ya mwaka wa 2012 ya Shirika la Afya Ulimwenguni, asilimia 63 ya vifo vilisababishwa na magonjwa ya kuambukiza, hasa UKIMWI, kuharisha, malaria, kifua kikuu, na magonjwa ya watoto.

Australia

Michezo ya kamari kwenye simu na vifaa vingine vya kielektroniki inapendwa sana na watoto. Baadhi ya michezo hiyo inafanana kabisa na michezo halisi ya kamari ingawa ni rahisi zaidi kushinda. Ripoti moja ya serikali inaonya kwamba michezo hiyo inaweza kufanya watoto waone kamari kuwa jambo la kawaida “na huenda ikawafanya wawe na tatizo la kucheza kamari watakapokuwa watu wazima.”