NCHI NA WATU
Kutembelea Uzbekistan
TRANSOXIANA. Nchi Katikati ya Mito. Tartary. Turkistan. Majina mengi yametumiwa ili kutambulisha eneo ambalo leo linatia ndani Uzbekistan, “Nchi ya Wauzbeki.” Tangu mapema karne ya 15, majiji ya Uzbekistan yaliwafaa wafanyabiashara waliosafiri katika barabara iliyounganisha China na Bahari ya Mediterania. Pamba hutumiwa zaidi katika viwanda vya nguo nchini humo. Mazulia mazuri yaliyotengenezwa kwa kutumia pamba, sufu, au hariri huuzwa pia.
Historia inaonyesha kwamba watu mbalimbali wamechangia utamaduni wa Uzbekistan. Watawala maarufu na majeshi yao yenye nguvu walipita katika milima na majangwa ya nchi ya Uzbekistan. Watu hao wanatia ndani Aleksanda Mkuu, aliyekutana na mpenzi wake Roxane; Genghis Khan, kutoka Mongolia; na Timur (anayejulikana pia kama Tamerlane), mwenyeji wa eneo hilo, aliyetawala mojawapo ya milki kubwa zaidi katika historia.
Minara yenye rangi zinazovutia yenye makuba yaliyofunikwa na vigae vyenye rangi ya bluu hufanya miji ya kisasa ya Uzbekistan ivutie. Majengo hayo mengi hutumiwa kama shule.
Barabara iliyounganisha China na Bahari ya Mediterania. Barabara hiyo ambayo inapita katika eneo ambalo leo ni Uzbekistan, ilikuwa maarufu sana katika ulimwengu wa biashara. Ilianza kutumiwa muda mrefu hadi njia mpya ya kwenda India kupitia bahari ilipofunguliwa mwishoni mwa karne ya 15 W.K.
Bahari ya Aral. Kwa kuwa mkondo wa maji ya Bahari ya Aral uligeuzwa na kutumiwa katika kilimo cha umwagiliaji—ambayo iliwahi kuwa ziwa la nne kwa ukubwa duniani—inaanza kutoweka. Nchi ya Uzbekistan inashirikiana na nchi zingine kutatua tatizo hilo.
Alfabeti za Uzbekistan zinazobadilika. Lugha mbalimbali zilitumiwa katika nchi hii lakini baada ya uvamizi wa Waislamu katika karne ya nane, Kiarabu kilianza kutumiwa. Baada ya nchi hii kuunga mkono Muungano wa Sovieti, alfabeti za Kilatini zilianza kutumiwa kwa mara ya kwanza na kisha herufi za Kisirili zikaanza kutumiwa mwishoni mwa miaka ya 1930. Mwaka wa 1993, sheria mpya iliyotungwa ilianzisha alfabeti za Uzbekistan inayotegemea maandishi ya Kilatini.