Tunaweza Kushinda Chuki!
Je, umewahi kuchukiwa?
Ikiwa hujawahi, huenda umewahi kuona watu wakionyesha chuki kwa njia moja au nyingine. Mara nyingi tunasikia habari kuhusu watu wanaochukiwa kwa sababu ya jamii yao, taifa lao, au kwa kuwa ni wapenzi wa jinsia moja. Matokeo ni kwamba serikali nyingi zinatunga sheria za kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyosababishwa na chuki.
Watu wanaochukiwa huwachukia wengine pia. Mara nyingi watu hao hulipiza kisasi na hivyo kuchochea chuki zaidi.
Huenda umewahi kubaguliwa, kudhihakiwa, kuambiwa maneno yasiyofaa, na kutishwa. Hata hivyo, mara nyingi chuki huonyeshwa kwa njia kubwa zaidi. Inaweza kusababisha ghadhabu, kuwanyanyasa wengine, uharibifu wa mali, kuwashambulia wengine, ubakaji, mauaji, au hata mauaji ya kimbari.
Gazeti hili litajibu maswali yafuatayo na kuonyesha jinsi tunavyoweza kushinda chuki:
Kwa nini watu wengi wana chuki?
Tunawezaje kushinda chuki?
Je, kuna wakati ambapo chuki haitakuwapo tena?