Miili Midogo, Mioyo Mikubwa
Miili Midogo, Mioyo Mikubwa
INGEKUWAJE kuzungumza na watu usiowajua juu ya Ufalme wa Mungu kama ungekuwa mwenye kimo cha sentimeta 76 tu? Laura anaweza kukueleza. Akiwa na umri wa miaka 33, hicho ndicho kimo chake, sentimeta 76 tu. Yeye na dadake María, mwenye umri wa miaka 24 na kimo cha sentimeta 86, wanaishi jijini Quito, Ekuado. Ebu watueleze vizuizi wanavyokabili katika huduma yao ya Kikristo.
“Ili kufika kwenye eneo letu la kuhubiri na kwenye mikutano ya Kikristo, sisi hutembea umbali wa nusu kilometa ili kupanda basi. Kutoka mahali ambapo sisi hushukia, sisi hutembea umbali wa nusu kilometa nyingine ili kupanda basi la pili. Kwa kusikitisha, njia hii ina mbwa watano wakali. Mbwa hutuogofya sana kwa sababu wanaweza kuonekana wakubwa kama farasi. Ili kuwafukuza ikihitajika, sisi hubeba fimbo ndefu, ambayo sisi huficha mahali fulani kabla ya kupanda basi ili tuweze kuitumia tutembeapo kurudi nyumbani.
“Kupanda basi ni hatua kubwa kihalisi kwetu. Sisi husimama juu ya mwinuko fulani wa udongo kwenye kituo cha basi ili tuweze kulipanda kwa urahisi zaidi. Madereva wengine husimamisha gari karibu na mwinuko huo, lakini wengine hawafanyi hivyo. Wakikosa kufanya hivyo, aliye mrefu kati yetu humsaidia yule mfupi kupanda. Kupata basi la pili huhitaji kwamba tuvuke barabara kuu yenye magari mengi—jitihada kubwa kwa miguu yetu mifupi. Kwa sababu ya ufupi wetu, mfuko mzito wa vitabu hufanya hali iwe ngumu zaidi. Ili kufanya mfuko uwe mwepesi, sisi hutumia Biblia ndogo na pia hupunguza kiasi cha fasihi tunachobeba.
“Sote wawili tumekuwa tukishughulika tu na mambo yetu tangu utotoni. Majirani wetu wanajua kwamba tulikuwa tukiogopa sana kuzungumza na watu tusiowajua. Hivyo, wao hushangaa na kuvutiwa kutuona tukibisha milango yao, na kwa kawaida wao hutusikiliza. Lakini maeneo ambako hatujulikani sana, watu hutuona tu kuwa mbilikimo; hivyo nyakati nyingine hawasikilizi ujumbe wetu kwa makini inavyostahili. Hata hivyo, kuhisi upendo wa Yehova hututia moyo tuendelee katika kazi ya kueneza evanjeli. Kutafakari andiko la Mithali 3:5, 6 pia hututia moyo.”
Kama Laura na María wanavyodhihirisha, kuvumilia licha ya kasoro za mwili kunaweza kumtukuza Mungu. Mtume Paulo alisali kwamba “mwiba [wake] katika mwili,” yamkini ugonjwa wa kimwili, uondolewe. Lakini Mungu akamwambia: “Fadhili yangu isiyostahiliwa yakutosha wewe; 2 Wakorintho 12:7, 9, 10) Miaka kadhaa baadaye Paulo aliandika: “Kwa mambo yote ninayo nguvu kwa njia ya yeye anipaye nguvu.”—Wafilipi 4:13.
kwa maana nguvu yangu inafanywa kamilifu katika udhaifu.” Naam, si lazima kasoro ya mwili iondolewe ili tuweze kumtumikia Mungu. Kumtegemea Mungu kabisa kwaweza kutusaidia kutumia hali zetu kadiri tuwezavyo. Kwa kuwa Paulo aliuona “mwiba katika mwili” kwa njia hiyo, yeye angeweza kusema: “Niwapo dhaifu, ndipo niwapo mwenye nguvu.” (Siku hizi, Mungu anatimiza kazi kubwa mno kupitia wanaume, wanawake, na watoto ambao wamejitoa kabisa kwake. Baadhi yao wamelemaa kwa njia fulani. Ingawa wote wanatumaini kuponywa katika Ufalme wa Mungu, wao hawangoji hadi Mungu awaondolee matatizo ndipo wajaribu kumtumikia.
Je, una udhaifu fulani wa kimwili? Jipe moyo! Kupitia imani yako unaweza kuwa miongoni mwa watu kama Paulo, Laura, na María. Kuhusu hao, inaweza kusemwa kama ilivyosemwa kuhusu wanaume na wanawake wenye imani wa nyakati za kale: “Kutoka hali dhaifu wakafanywa wenye nguvu.”—Waebrania 11:34.
[Picha katika ukurasa wa 8, 9]
María
Laura
[Picha katika ukurasa wa 9]
María amsaidia Laura kupanda basi
[Picha katika ukurasa wa 9]
“Mbwa hutuogofya sana kwa sababu wanaweza kuonekana wakubwa kama farasi”
Chini: Laura na María na wale waliojifunza Biblia pamoja nao