Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

“Hatimaye Nimetambua Tatizo Langu!”

“Hatimaye Nimetambua Tatizo Langu!”

“Hatimaye Nimetambua Tatizo Langu!”

NDIVYO alivyohisi mwanamume mmoja huko Tokyo aliposoma simulizi la maisha katika toleo la Mnara wa Mlinzi la Desemba 1, 2000. Makala hiyo ilikuwa na kichwa, “Hamjui Uhai Wenu Utakuwa Nini Kesho,” na ilisimulia jambo lililompata mtu mmoja aliyekuwa mishonari ambaye anaugua ugonjwa unaoitwa manic-depressive psychosis (ugonjwa wa akili wa kushuka moyo na kusisimka-sisimka ghafula).

Mwanamume huyo kutoka Tokyo alisema hivi katika barua aliyowaandikia wachapishaji wa gazeti hili: “Dalili zilizoelezwa za ugonjwa huo zafanana na zangu kabisa. Kwa hiyo nilienda katika hospitali ya matibabu ya akili kisha ikagunduliwa kwamba nina ugonjwa wa manic depression. Daktari aliyenipima alishangaa. Alisema, ‘Ni nadra sana kwa watu walio na ugonjwa huu kutambua kwamba ni wagonjwa.’ Nilisaidiwa kuujua ugonjwa huo kabla haujawa mbaya sana.”

Mamilioni ya watu ulimwenguni pote hunufaika katika njia mbalimbali kwa kusoma kila toleo la gazeti la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Wanaona makala hizo kuwa zenye kuelimisha na kuthawabisha. Sasa gazeti Mnara wa Mlinzi huchapishwa katika lugha 141, nalo Amkeni! huchapishwa katika lugha 86. Wewe pia utafurahia kusoma gazeti la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwa ukawaida.