Mti Unaotoa “Machozi” Yenye Matumizi Mengi
Mti Unaotoa “Machozi” Yenye Matumizi Mengi
Andiko la Yeremia 51:8, “Zaire Swahili Bible” husema: “Twaeni mafuta ya zeri kwa maumivu.” Twasafiri kwa njia ya mfano hadi kisiwa cha Chios, katika Bahari ya Aegea ili kutafuta mojawapo ya asili ya mafuta haya yenye kutuliza na kuponya.
MAPEMA wakati wa kiangazi, wakulima wa Chios hujitayarisha kuvuna kwa njia isiyo ya kawaida. Baada ya kufagia, wao hujenga mwinuko tambarare kwa udongo mweupe chini ya mimea ya kijani kibichi inayoitwa mastic (miti inayotoa utomvu). Kisha wakulima hupasua maganda ya miti hiyo na kufanya “itoe machozi.” “Machozi” ya utomvu wa rangi nyeupe-nyeupe huanza kutiririka. Baada ya majuma mawili au matatu, matone ya utomvu huo huganda kisha wakulima huyachukua ama moja kwa moja kutoka kwenye shina au kwenye udongo mweupe. “Machozi” hayo yanayoitwa masticha, yanatumiwa kutengeneza zeri.
Hata hivyo, kabla ya mavuno, saburi na kazi ngumu inahitajiwa. Mti huo wenye shina la rangi ya kijivujivu lililojipinda-pinda hukua polepole sana nao huchukua muda wa miaka 40 hadi 50 ili kukomaa kabisa—kwa kawaida hufikia urefu wa meta 2 hadi 3.
Mbali na kazi ya kupasua mashina na kukusanya “machozi,” lazima kazi zaidi ifanywe ili kutokeza utomvu. Baada ya wakulima kukusanya “machozi” ya utomvu, wanayapepeta, kuyasafisha, na kuyachagua kulingana na ukubwa na ubora wake. Baadaye, utomvu husafishwa kisha unaweza kutumiwa kwa kazi mbalimbali.
Historia ya Mmea huo Wenye Thamani
Neno linalotumiwa na Wagiriki kufafanua utomvu linamaanisha “kusaga meno.” (Mathayo 8:12; Ufunuo 16:10) Jina hilo ladokeza kwamba tangu zamani, utomvu umekuwa ukitumiwa kama chingamu kufanya pumzi iwe safi.
Herodotus, mwanahistoria Mgiriki wa karne ya tano K.W.K., ndiye aliyekuwa wa kwanza kuandika kuhusu utomvu. Waandishi na madaktari wengine wa kale—kutia ndani Apollodorus, Dioscorides, Theophrastus, na Hippocrates—walitaja matumizi ya kitiba ya utomvu. Ijapokuwa miti hii ya mastic inayotoa utomvu hukua kotekote katika Pwani ya Mediterania, tangu mwaka wa 50 W.K. hivi, miti hiyo imekuwa ikipandwa katika eneo la Chios pekee. Waroma, Wagenoa, na Waturuki walimiliki eneo la Chios kwa kuwa walivutiwa na miti hiyo inayotoa utomvu.
Utomvu Wenye Matumizi Mengi
Madaktari wa kale wa Misri walitumia utomvu kutibu magonjwa mbalimbali, kutia ndani kuharisha na yabisi-kavu. Waliutumia pia kama uvuYeremia 8:22; 46:11) Hata inadhaniwa kwamba mti huo unaotoa natafi, mojawapo ya vitu vilivyotumiwa kutengeneza manukato ya uvumba mtakatifu uliotumiwa kwa makusudi matakatifu pekee, huenda ukawa wa jamii ya miti inayotoa utomvu.—Kutoka 30:34, 35.
mba na dawa ya kuhifadhi maiti. Huenda mti unaotoa utomvu ukawa ndio asili ya ‘mafuta ya zeri ya Gileadi’ yanayotajwa katika Biblia ambayo yalitumiwa kama dawa, kutengeneza vipodozi, na kuhifadhi maiti. (Leo, utomvu hutumiwa kutengeneza vanishi zinazozuia picha zilizochorwa kwa rangi ya mafuta , fanicha, na ala za muziki zisichakae. Hutumiwa kutengeneza vifaa vya kuzuia umeme na maji yasipenye, na ni mojawapo ya vitu bora zaidi vinavyohifadhi rangi za nguo na za kuchora. Pia utomvu hutumiwa katika gundi na kufanya ngozi isioze. Kwa sababu ya harufu yake yenye kupendeza, utomvu hutumiwa kutengeneza sabuni, vipodozi, na marashi.
Utomvu umetajwa katika orodha rasmi 25 za dawa zinazokubaliwa ulimwenguni pote. Bado unatumiwa sana kama dawa ya kienyeji katika nchi za Uarabu. Utomvu hutumiwa pia katika vitu vya kuziba meno na hupakwa ndani ya gamba la dawa.
Mti unaotoa “machozi” yenye matumizi mengi na ambao ndio asili ya zeri, umetuliza na kuponya watu kwa karne nyingi. Kwa sababu nzuri, unabii wa Yeremia husema: “Twaeni mafuta ya zeri kwa maumivu.”
[Picha katika ukurasa wa 31]
Chios
Kuvuna utomvu
“Machozi” ya mti huo yakusanywa kwa uangalifu
[Hisani]
Chios na picha ya mavuno: Courtesy of Korais Library; picha nyingine zote: Kostas Stamoulis