Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mtu Yeyote Anaweza Kuwa Mlemavu

Mtu Yeyote Anaweza Kuwa Mlemavu

Mtu Yeyote Anaweza Kuwa Mlemavu

CHRISTIAN, anayeishi katika nchi moja ya Afrika, alitekwa nyara na wanajeshi waliojaribu kumlazimisha ajiunge na jeshi, lakini kwa sababu ya dhamiri yake iliyozoezwa na Biblia akakataa. Kisha wanajeshi hao wakampeleka katika kambi ya kijeshi, na baada ya kupigwa kwa siku nne, mmoja wao akampiga risasi mguuni. Ijapokuwa Christian alifaulu kufika hospitalini, ilikuwa lazima mguu wake ukatwe chini ya goti. Katika nchi nyingine ya Afrika, hata watoto wachanga wamekatwa miguu na mikono yao na waasi wenye silaha. Na mabomu yaliyotegwa chini ya ardhi yanaendelea kuwaumiza na kuwalemaza wazee kwa vijana huko Afghanistan, Angola, Balkani, na Kambodia.

Aksidenti na magonjwa kama vile ugonjwa wa sukari, yamesababisha kuongezeka kwa ulemavu pia. Hata sumu katika mazingira inaweza kulemaza. Kwa mfano, karibu na jiji moja la Ulaya Mashariki, watoto kadhaa wamezaliwa bila sehemu ya chini ya mmojawapo wa mikono yao. Wana sehemu fupi tu ya mkono, kuanzia kiwiko kwenda juu. Ni wazi kwamba uchafuzi unaosababishwa na kemikali hudhuru chembe chembe za urithi. Watu wengine wengi bado wana miguu na mikono lakini ni walemavu kwa sababu ya kupooza au matatizo mengineyo. Bila shaka mtu yeyote anaweza kuwa mlemavu.

Hata uwe umesababishwa na nini, ulemavu huvunja moyo sana. Akiwa na umri wa miaka 20, Junior alikatwa mguu wa kushoto. Baadaye alisema hivi: “Nilitatizika sana kihisia. Kujua kwamba sitakuwa na mguu wangu tena, kulifanya nilie sana. Sikujua la kufanya. Nilichanganyikiwa.” Hata hivyo, baadaye maoni ya Junior yalibadilika sana. Alianza kujifunza Biblia na kujua mambo ambayo yamemsaidia kukabiliana na ulemavu wake na kumpa tumaini bora la wakati ujao wenye furaha hapa duniani. Iwapo wewe ni mlemavu, je, ungependa kuwa na tumaini kama hilo?

Ikiwa ndivyo, tafadhali soma makala inayofuata. Tunapendekeza utumie Biblia yako mwenyewe kusoma Maandiko yaliyoonyeshwa ili ujionee yale ambayo Muumba amewaahidi wale wanaojifunza kuhusu makusudi yake na kuishi kulingana nayo.