Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kapadokia—Mahali Ambapo Watu Waliishi Katika Nyumba Zilizochongwa na Upepo na Maji

Kapadokia—Mahali Ambapo Watu Waliishi Katika Nyumba Zilizochongwa na Upepo na Maji

Kapadokia—Mahali Ambapo Watu Waliishi Katika Nyumba Zilizochongwa na Upepo na Maji

MTUME Petro alitaja Kapadokia. Kati ya watu aliowaandikia barua yake ya kwanza iliyoongozwa na roho ya Mungu ni “wakaaji wa muda waliotawanyika huku na huku katika . . . Kapadokia.” (1 Petro 1:1) Kapadokia ilikuwa nchi ya aina gani? Kwa nini wakaaji wake waliishi kwenye nyumba zilizochongwa katika mawe? Ukristo uliwafikiaje?

Msafiri Mwingereza, W. F. Ainsworth, aliyetembelea Kapadokia miaka ya 1840, alisema, “Kwa ghafula tulijikuta katika eneo lenye nguzo na mawe mengi yenye umbo la pia.” Mandhari hii isiyo ya kawaida huwashangaza wageni wa siku hizi ambao hutembelea eneo hili la Uturuki. Kwenye mabonde ya Kapadokia kuna “sanamu” za mawe zisizo za kawaida zilizokaribiana na ambazo hazitoi sauti yoyote. Nyingine ni kama mabomba makubwa ya kutolea moshi yenye urefu wa meta 30 au zaidi. Nyingine zinafanana na koni za aiskrimu, minara, au uyoga.

Jua huangaza juu ya sanamu hizo na kutokeza rangi mbalimbali zenye kuvutia wakati tofauti-tofauti wa siku! Kwenye mapambazuko zinakuwa na rangi ya waridi isiyokolea. Mchana zinakuwa na rangi ya kijivu-jivu isiyokolea, na wakati jua linapotua, zinakuwa na rangi ya kahawia na manjano. Ni nini kilichofanyiza “nguzo hizo na mawe hayo mengi yenye umbo la pia”? Na kwa nini watu wa eneo hilo walichonga nyumba zao ndani ya mawe hayo?

Zilichongwa na Upepo na Maji

Eneo la Kapadokia liko katikati ya Peninsula ya Anatolia, ambayo inaunganisha Asia na Ulaya. Eneo hili lingekuwa uwanda wa juu ulio tambarare kama halingekuwa na volkeno mbili. Miaka mingi iliyopita, milipuko mikubwa sana ya volkeno ilifunika eneo hilo kwa mawe aina mbili—meusi magumu na meupe mororo, ambayo hutokea baada ya jivu la volkeno kukauka na kuwa gumu.

Baada ya mito, mvua, na upepo kumomonyoa mawe hayo mororo, korongo zilifanyizwa. Mwishowe, baadhi ya majabali yaliyo karibu na makorongo hayo yalivunjika na kutokeza nguzo nyingi sana za mawe yenye umbo la pia na kufanya nchi hiyo iwe na sanamu ambazo hazipatikani mahali penginepo duniani. Baadhi ya mawe hayo yenye umbo la pia yalikuwa na matundu mengi sana hivi kwamba yalifanana na sega la asali. Wenyeji walichonga vyumba kwenye mawe hayo mororo na kuongezea vyumba vingine familia ilipokuwa kubwa. Pia waliona makao hayo kuwa yenye baridi wakati wa kiangazi na yenye joto wakati wa majira ya baridi kali.

Kuishi Mahali Penye Ustaarabu

Yaelekea kama wakaaji wa mapango wa Kapadokia hawangeishi mahali muhimu penye ustaarabu, hawangechangamana sana na watu wengine. Barabara maarufu iliyoitwa Silk Road—yenye urefu wa kilometa 6,500—iliyotumiwa na wafanyabiashara, na ambayo iliunganisha Milki ya Roma na China, ilipitia Kapadokia. Mbali na wafanyabiashara, majeshi ya Waajemi, Wagiriki, na Waroma yalitumia barabara hiyo. Wasafiri hao walileta imani mpya za kidini.

Kufikia karne ya pili K.W.K., kulikuwa na jamii za Wayahudi huko Kapadokia. Na Wayahudi kutoka eneo hilo walikuweko Yerusalemu mnamo mwaka wa 33 W.K. Walikuwa huko ili kusherehekea Sherehe ya Pentekoste. Hivyo, mtume Petro aliwahubiria Wayahudi wa Kapadokia baada ya roho takatifu kumwagwa. (Matendo 2:1-9) Yaelekea baadhi yao walikubali ujumbe wake na wakawaeleza wenzao imani yao mpya waliporudi makwao. Hivyo, katika barua yake ya kwanza Petro alikuwa akizungumza na Wakristo wa Kapadokia.

Hata hivyo, baada ya muda, Wakristo wa Kapadokia walianza kuathiriwa na falsafa za wapagani. Hata viongozi watatu mashuhuri wa kanisa ambao ni wenyeji wa Kapadokia wa karne ya nne walitetea kwa bidii fundisho la Utatu lisilopatana na Maandiko. Viongozi hao ni Gregory wa Nazianzus, Basil Mkuu, na ndugu yake Gregory wa Nyssa.

Pia Basil Mkuu aliwatia watu moyo waishi maisha ya kitawa. Nyumba za hali ya chini za wakaaji wa Kapadokia ambazo zilichongwa katika mawe, zilifaa sana kwa ajili ya maisha yaliyopendekezwa na Basil. Jamii hiyo ya watawa ilipokua, makanisa yalijengwa ndani ya mawe makubwa zaidi yenye umbo la pia. Kufikia karne ya 13, makanisa mia tatu hivi yalikuwa yamechongwa katika mawe. Mengi ya makanisa hayo yamehifadhiwa hadi leo.

Ingawa makanisa hayo na makao ya watawa hayatumiki tena, mtindo wa maisha wa wenyeji haujabadilika sana kwa karne nyingi. Bado mapango mengi yanatumiwa kama makao. Watu wengi ambao hutembelea Kapadokia hushangaa kuona jinsi wakaaji hao werevu walivyotengeneza nyumba kutokana na uumbaji wa asili.

[Ramani katika ukurasa wa 24, 25]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

KAPADOKIA

CHINA (Cathay)