Mti wa Mwaka Mpya—Ni Desturi ya Urusi au ya Kikristo?
Mti wa Mwaka Mpya—Ni Desturi ya Urusi au ya Kikristo?
“MWANZONI mwa miaka ya 1830, mti wa kijani [wa sherehe] ulionwa kuwa ‘desturi ya Kijerumani yenye kuvutia.’ Mwishoni mwa miaka ya 1830, mti huo ulianza kutumiwa ‘kwa ukawaida’ katika nyumba za matajiri huko St. Petersburg. . . . Ni makasisi tu na watu wa hali ya chini ambao hawakuweka mti huo katika nyumba zao katika karne ya 19. . . .
“Kabla ya wakati huo, mti huo, . . . haukupendwa. Mabadiliko katika maoni ya watu yaliyotukia katikati ya karne ya 19 yalitofautiana na desturi za Warusi ambao waliuona mti huo kuwa ishara ya kifo na kuuhusianisha na ‘ulimwengu wa roho,’ nayo yalitofautiana pia na ile desturi ya kuuweka juu ya mapaa ya nyumba za kuuza kileo. . . . Inaeleweka kabisa kwamba katika jitihada za kufanya zoea la kurembesha nyumba kwa mti huo likubaliwe, desturi hiyo ya kigeni ingeonwa kama vile mti wa Krismasi ulivyoonwa huko Magharibi, yaani, ungehusianishwa na wazo kuu la Krismasi. . . .
“Jitihada za kufanya mti huo uwe ishara ya Kikristo zilikabili upinzani huko Urusi. Zilipingwa na Kanisa Othodoksi. Makasisi waliona sherehe hiyo mpya kuwa na ‘uvutano wa kishetani,’ yaani, waliiona kuwa desturi ya kipagani ambayo haikuwa na uhusiano wowote na kuzaliwa kwa Mwokozi, na isitoshe, ilikuwa desturi iliyotoka Magharibi.”—Profesa Yelena V. Dushechkina, mtaalamu wa elimu ya lugha kwenye Chuo Kikuu cha Taifa cha St. Petersburg.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]
Photograph: Nikolai Rakhmanov