Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

 HABARI KUU | JE, SHETANI NI KIUMBE HALISI?

Je, Kuna Shetani?

Je, Kuna Shetani?

Mchongo jijini Madrid, Hispania, unaoonyesha Shetani kama malaika mwovu

“Nilizaliwa na kulelewa nchini El Salvador. Mama yangu aliniambia hivi nilipokosea: ‘Shetani anakuja kukuchukua!’ Mimi nilimjibu, ‘Mwache aje!’ Nilimwamini Mungu, sikuamini kuna Shetani.”—ROGELIO.

Je, unakubaliana na Rogelio? Unakubaliana na ipi kati ya hoja zifuatazo?

  • Hakuna Shetani; bali ni alama tu ya kuwakilisha uovu.

  • Shetani yupo, lakini hajihusishi na mambo ya wanadamu.

  • Shetani ni kiumbe wa roho mwenye nguvu ambaye huwashawishi wanadamu.

Kila mojawapo ya hoja hizo inaungwa mkono na watu wengi. Lakini je, ni muhimu kujua jibu sahihi? Ikiwa hakuna Shetani, basi wale wanaosema kuna Shetani wamepotoshwa. Ikiwa Shetani yupo lakini hajihusishi na wanadamu, basi hakuna haja ya kuogopa. Hata hivyo, ikiwa Shetani anashawishi na kupotosha watu, basi yeye ni kiumbe hatari kuliko wengi wanavyodhani.

Acheni tuchunguze jinsi Maandiko Matakatifu yanavyojibu maswali yafuatayo: Shetani ni nani au ni nini? Je, ni alama ya uovu au kiumbe wa roho? Ikiwa ni kiumbe wa roho, je, anaweza kukudhuru? Ikiwa ndivyo, unawezaje kujilinda?