Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Chris McGrath/Getty Images

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Vita?

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Vita?

KAMPENI YA PEKEE

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Vita?

 Ulimwengu unaendelea kuathiriwa na vita vinavyosababisha maumivu na kuteseka kwingi. Ona ripoti zifuatazo:

  •   “Tarakimu mpya zinaonyesha kwamba idadi ya watu waliokufa kutokana na vita imeongezeka kuliko miaka 28 iliyopita, hasa kwa sababu ya vita vinavyoendelea nchini Ethiopia na pia Ukrainia.”​—Taasisi ya Utafiti Kuhusu Amani ya Oslo, Juni 7, 2023.

  •   “Vita nchini Ukrainia ni moja tu kati ya vita vilivyoongezeka katika mwaka wa 2022. Kwa ujumla, mwaka uliopita jeuri inayosababishwa na mambo ya kisiasa iliongezeka kwa asilimia 27 ulimwenguni pote. Inakadiriwa kwamba watu bilioni 1.7 waliathiriwa na madhara ya vita.”​—The Armed Conflict Location & Event Data Project (ACLED), Februari 8, 2023.

 Biblia inatupatia tumaini. Inasema kwamba “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa kamwe.” (Danieli 2:44) Ufalme, au serikali hiyo itakapotawala, Mungu ‘atakomesha vita katika dunia yote.’​—Zaburi 46:9