Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

TheCrimsonMonkey/E+ via Getty Images

KAMPENI YA PEKEE

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Uharibifu wa Mazingira?

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Uharibifu wa Mazingira?

 “Hali ya hewa imezorota sana na matokeo ni kwamba viumbe hai, miji, na watu wamepata madhara makubwa. Ulimwenguni pote, mabadiliko ya hali ya hewa yanatokeza dhoruba kubwa zinazoharibu nyumba za watu na kuvuruga shughuli wanazofanya ili kupata riziki. Hali ya joto inazidi kuongezeka baharini, kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa aina nyingi za samaki na wanyama wanaoishi baharini kufa.”​—Inger Andersen, msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa. Pia ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Julai 25, 2023.

 Je, serikali zitashirikiana ili kupambana na masuala haya yanayoathiri ulimwengu mzima? Je, kweli wana uwezo wa kutatua matatizo haya?

 Biblia inatueleza kwamba kuna serikali yenye uwezo wa kutatua uharibifu wa mazingira. Kwa hakika, serikali hiyo itatatua tatizo hilo. Biblia inasema kwamba “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme,” yaani, serikali ambayo itatawala dunia na kutatatua matatizo yote yalipo. (Danieli 2:44) Chini ya utawala huo watu “hawatasababisha madhara yoyote wala uharibifu wowote” iwe ni kwa mtu mwingine au kwa dunia yenyewe.​—Isaya 11:9.