Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Comstock Images/Stockbyte via Getty Images

KAMPENI YA PEKEE

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuwahusu Viongozi Wafisadi?

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuwahusu Viongozi Wafisadi?

 Watu wamechoshwa na wanasiasa wafisadi, wanataka viongozi ambao wanaaminika. Katika utafiti mmoja uliofanywa sehemu mbalimbali ulimwenguni mwaka wa 2023, viongozi wa kisiasa walishika namba moja kati ya watu ambao hawaaminiki. a

 Biblia inaeleza kwamba kuna serikali ambayo Kiongozi wake anaaminika kabisa, ni mnyoofu, na hana ufisadi. Serikali hiyo ni Ufalme wa Mungu na Kiongozi wake ni Yesu Kristo.​—Isaya 9:7.

 Yesu amethibitisha kwa matendo kwamba anawajali watu kutoka moyoni. (Mathayo 9:35, 36) Akiwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu atahakikisha kwamba raia wake wote wanapata haki na wanaishi kwa amani.​—Zaburi 72:12-14.

a Ripoti ya Ulimwenguni Pote ya 2023 Iliyotayarishwa na Shirika la Edelman Trust Barometer.