Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Brais Seara/Moment via Getty Images

ENDELEA KUKESHA!

Ukame Unaoongozeka​—Biblia Inasema Nini?

Ukame Unaoongozeka​—Biblia Inasema Nini?
  •   “China imeripoti kwamba nchini humo mwaka huu kulikuwa na majira ya kiangazi yenye ‘kiwango cha juu zaidi’ cha joto na yenye ukame sana. Hii ni mara ya tatu katika rekodi yao kuwa na majira yenye ukame kwa kiwango hicho.”​—The Guardian, Septemba 7, 2022.

  •   ‘Inakadiriwa kwamba ukame ulio katika upande wa Mashariki wa bara la Afrika utaendelea kwa mwaka wa tano mfululizo.’​—UN News, Agosti 26, 2022.

  •   “Zaidi ya nusu ya bara la Ulaya inakabili ukame, na inaelekea huo ndio ukame mbaya zaidi kupata maeneo hayo katika kipindi cha miaka 500.”​—BBC News, Agosti 23, 2022.

 Wataalamu wengi wanatabiri kwamba ukame kama huo utaendelea kuwepo au utakuwa mbaya hata zaidi. Je, kuna tumaini lolote kwamba hali zitakuwa nzuri? Biblia inasema nini?

Ukame Katika Unabii wa Biblia

 Biblia ilitabiri hivi kuhusu siku zetu:

  •   “Kutakuwa na . . . upungufu wa chakula katika sehemu mbalimbali.”​—Luka 21:11.

 Mara nyingi ukame husababisha upungufu wa chakula. Upungufu wa chakula pamoja na mateso na vifo vinavyotokana na tatizo hilo hutimiza unabii wa Biblia.​—Ufunuo 6:6, 8.

Kwa nini ukame unaongezeka?

 Biblia inafunua sababu ya msingi inayofanya ukame uongezeke. Inasema:

  •   “Mwanadamu anayetembea hana uwezo wa kuongoza hatua yake.”​—Yeremia 10:23.

 Hilo linamaanisha kwamba wanadamu hawawezi “kuongoza hatua [yao],” au kujitawala kwa mafanikio. Mara nyingi maamuzi mabaya wanayofanya husababisha ukame na upungufu wa maji.

  •   Wanasayansi wengi hukubali kwamba shughuli za wanadamu husababisha kuongezeka kwa hali ya joto duniani, na hilo husababisha ukame kuongezeka katika sehemu mbalimbali ulimwenguni.

  •   Pupa na sera zenye manufaa ya muda mfupi zimesababisha ukataji wa miti, uchafuzi wa mazingira, matumizi mabaya ya rasilimali, na mambo hayo huharibu vyanzo vya maji.

 Hata hivyo, Biblia inatupatia tumaini.

Je, kuna tumaini lolote kwamba hali zitakuwa nzuri?

 Biblia inasema kwamba Mungu ataondoa tatizo la upungufu wa maji. Jinsi gani?

  1.  1. Mungu “[atawaharibu] wale wanaoiharibu dunia.” (Ufunuo 11:18) Ataondoa chanzo kimoja cha upungufu wa maji, yaani, atawaangamiza watu waovu na wenye pupa ambao hufanya mambo yanayoharibu mazingira.​—2 Timotheo 3:1, 2.

  2.  2. “Ardhi iliyokaushwa na joto itakuwa kama dimbwi lenye matete.” (Isaya 35:1, 6, 7) Mungu ataondoa kabisa madhara yaliyosababishwa na ukame na atafanya dunia kuwa paradiso na itakuwa na maji ya kutosha.

  3.  3. “Unaitunza dunia, unaifanya izae kwa wingi na kuitajirisha sana.” (Zaburi 65:9) Kwa baraka za Mungu, dunia itakuwa na chakula kingi kizuri na maji safi kwa ajili ya wote.