WIMBO NA. 148
Yehova Huokoa
-
1. Yehova Mungu wetu uliye hai.
Kazi zako kuu,
mbingu na dunia.
Ndiwe Mungu pekee, Mweza-yote
—milele.
Wakujue wewe.
(KORASI)
Yehova huokoa wa’minifu.
Wamwone kuwa Mungu wa nguvu nyingi.
Kwa bidii na ujasiri
sisi sote,
Twatangaza jina kuu
lake Yehova.
-
2. Japo kuna kifo, nakutegemea,
“Yehova unipe,
ujasiri, nguvu.”
Toka hekalu lako,
usikie, ‘Nifiche,
Niokoe, Mungu.’
(KORASI)
Yehova huokoa wa’minifu.
Wamwone kuwa Mungu wa nguvu nyingi.
Kwa bidii na ujasiri
sisi sote,
Twatangaza jina kuu
lake Yehova.
-
3. Utakaponguruma
kutoka juu.
Maadui wako,
waingiwe hofu.
Wakutumikiao, wafurahi.
Wajue
U Mwokozi wetu.
(KORASI)
Yehova huokoa wa’minifu.
Wamwone kuwa Mungu wa nguvu nyingi.
Kwa bidii na ujasiri
sisi sote,
Twatangaza jina kuu
lake Yehova.
(Ona pia Zab. 18:1, 2; 144:1, 2.)