WIMBO NA. 16
Msifuni Yah kwa Mwana Wake Mtiwa Mafuta
-
1. Yehova ameteua,
Mwanaye atawale.
Ana haki ya kutawala,
Mapenzi yatatendeka.
(KORASI)
Enyi Kondoo, Msifuni
Yehova na Kristo Yesu,
Mfuateni siku kwa siku,
na kumtii yeye.
Msifuni Yah kwa Mfalme,
mtiwa-mafuta wake,
atakayelitukuza jina
la Mungu takatifu.
-
2. Yehova ameteua,
Ndugu za Kristo Yesu.
Watawale pamoja naye,
Na kuleta Paradiso.
(KORASI)
Enyi Kondoo, Msifuni
Yehova na Kristo Yesu,
Mfuateni siku kwa siku,
na kumtii yeye.
Msifuni Yah kwa Mfalme,
mtiwa-mafuta wake,
atakayelitukuza jina
la Mungu takatifu.
(Ona pia Met. 29:4; Isa. 66:7, 8; Yoh. 10:4; Ufu. 5:9, 10.)