WIMBO NA. 22
Ufalme Umesimamishwa—Na Uje!
-
1. Yehova Mungu Mkuu
Mungu wa Milele
Umemtawaza Kristo
Awe mtawala.
Ufalme umezaliwa;
Utatawala dunia.
(KORASI)
Sasa kumekuwa
Wokovu, nguvu, Ufalme.
Umesimamishwa.
Twasali: ‘Ufalme Uje’
-
2. Karibuni Ibilisi
Ataondolewa.
Ingawa ole zazidi,
Hatuko gizani.
Ufalme umezaliwa;
Utatawala dunia.
(KORASI)
Sasa kumekuwa
Wokovu, nguvu, Ufalme.
Umesimamishwa.
Twasali: ‘Ufalme Uje’
-
3. Malaika wa mbinguni
Wanashangilia.
Shetani katupwa chini;
Mbingu zafurahi,
Ufalme umezaliwa;
Utatawala dunia.
(KORASI)
Sasa kumekuwa
Wokovu, nguvu, Ufalme.
Umesimamishwa.
Twasali: ‘Ufalme Uje’
(Ona pia Dan. 2:34, 35; 2 Kor. 4:18.)