WIMBO NA. 62
Wimbo Mpya
-
1. Mwimbie Mungu, wimbo mpya kwa furaha;
Tangaza matendo yote afanyayo.
Msifu yeye, Ndiye Mungu wa ushindi;
Anapohukumu,
hutenda kwa haki.
(KORASI)
Imbeni!
Twimbe wimbo mpya.
Imbeni!
Yehova Mfalme.
-
2. Shangilieni, pigeni vigelegele;
Jina lake sifu, na kumtukuza.
Jiunge nasi, tumwimbie Bwana wetu,
Piga tarumbeta,
kinubi na zeze.
(KORASI)
Imbeni!
Twimbe wimbo mpya.
Imbeni!
Yehova Mfalme.
-
3. Bahari navyo vilivyomo vimsifu,
Uumbaji wote umwimbie sifa.
Mito, vijito, vyote vipige makofi,
Milima, vilima,
vimsifu Yeye.
(KORASI)
Imbeni!
Twimbe wimbo mpya.
Imbeni!
Yehova Mfalme.
(Ona pia Zab. 96:1; 149:1; Isa. 42:10.)