Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 77

Nuru Katika Ulimwengu Wenye Giza

Nuru Katika Ulimwengu Wenye Giza

(2 Wakorintho 4:6)

  1. 1. Twaishi, siku za giza,

    Nuru twaiona.

    Ni kama mapambazuko,

    Punde asubuhi.

    (KORASI)

    Mwangaza gizani;

    Ujumbe wa Ufalme.

    Tumaini zuri—

    Giza latoweka,

    Nuru yaonekana—

    Mwanzo mpya.

  2. 2. Walio usingizini,

    Muda wayoyoma.

    Tuwape habari njema,

    Wapate uzima.

    (KORASI)

    Mwangaza gizani;

    Ujumbe wa Ufalme.

    Tumaini zuri—

    Giza latoweka,

    Nuru yaonekana—

    Mwanzo mpya.