Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 153

Nipe Ujasiri

Nipe Ujasiri

(2 Wafalme 6:16)

  1. 1. Nina shaka, woga;

    Sijui yajayo.

    Yehova waniongoza;

    U karibu nami!

    Japo si rahisi,

    Sina shaka kamwe:

    Yah U mshikamanifu;

    Ni salama kwako!

    (KORASI)

    Yehova, nipe imani,

    Nipate kuona,

    Jeshi kubwa lililo nasi.

    Nisiwe na woga.

    Nipe ujasiri;

    Yote nihimili.

    Naomba ujasiri.

    Ushindi ni Wako!

  2. 2. Hofu hunipata,

    Nami ni dhaifu.

    Mwamba wangu, ngome yangu;

    Mungu mweza yote.

    Nipe ujasiri,

    Na moyo hodari.

    Nisiogope chochote:​—

    Gereza, kaburi.

    (KORASI)

    Yehova, nipe imani,

    Nipate kuona,

    Jeshi kubwa lililo nasi.

    Nisiwe na woga.

    Nipe ujasiri;

    Yote nihimili.

    Naomba ujasiri.

    Ushindi ni Wako!

    (KORASI)

    Yehova, nipe imani,

    Nipate kuona,

    Jeshi kubwa lililo nasi.

    Nisiwe na woga.

    Nipe ujasiri;

    Yote nihimili.

    Naomba ujasiri.

    Ushindi ni Wako!

    Naomba ujasiri.

    Ushindi ni Wako!