Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mpe Yehova Utukufu

Mpe Yehova Utukufu

(Zaburi 96:8)

Pakua:

  1. 1. Mwenye enzi, Ee Yehova,

    Ukiwa ju’ mbinguni.

    Naweza kukupa nini

    Kwa upendo wako mwingi?

    Nitazamapo angani,

    Naona nguvu zako.

    Mimi ni nani Yehova,

    Unipe kibali chako?

    (KORASI)

    Ee Yehova, ninakuimbia.

    Wimbo wa kukusifu.

    Mungu wangu, mfalme milele,

    Unastahili sifa;

    Utukufu ni wako.

  2. 2. Maisha yangu nakupa.

    Nitakusifu wewe.

    Kutangaza njia zako

    Na kusema wema wako.

    Najivunia Yehova,

    Kukuabudu wewe.

    Wanipa nguvu na shangwe,

    Uniongoze milele.

    (KORASI)

    Ee Yehova, ninakuimbia.

    Wimbo wa kukusifu.

    Mungu wangu, mfalme milele,

    Unastahili sifa;

    Utukufu ni wako.

  3. 3. Mabonde mito bahari,

    Jua mwezi na nyota

    Hunista’jabisha mimi

    Upendo bila kifani.

    Hekima na utukufu:

    Naona mambo hayo.

    Kwa nini nisikusifu

    Kwa vyote ulivyoumba?

    (KORASI)

    Ee Yehova, ninakuimbia.

    Wimbo wa kukusifu.

    Mungu wangu, mfalme milele,

    Unastahili sifa;

    Utukufu ni wako.