Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Tua na Uanze Upya

Tua na Uanze Upya

Pakua:

  1. 1. Ni usiku mwangavu nyota zinameta,

    Tunaacha nyuma shida za siku, twawaza ya moyoni.

    Vema kuwa na muda wa kutafakari.

    Kushukuru—sana kwa zawadi zake—twathamini sana.​

    (KORASI)

    Na tutue kidogo tuone vema,

    Tutue na kutafakari

    Mambo ya muhimu, shangwe ya kutua,

    Kushusha pumzi,

    Anza upya.

  2. 2. Mwezi unapoangaza usiku wa manane,

    Tunahisi shangwe kwa zawadi bora kutoka kwa Baba ju’.

    Hata tukiwa na shida tutazame mbele,

    Tutavumilia tukijua kwamba Yehova atupenda.

    (KORASI)

    Na tutue kidogo tuone vema,

    Tutue na kutafakari

    Mambo ya muhimu, shangwe ya kutua,

    Kushusha pumzi,

    Anza upya.

    Anza upya;

    Anza upya.

    (KORASI)

    Tunatua kidogo tuone vema,

    Tutue na kutafakari

    Mambo muhimu, shangwe ya kutua,

    Kushusha pumzi,

    Anza upya.

    (UMALIZIO)

    Onja utamu; ona vema.

    Na shusha pumzi.

    Onja utamu; ona vema.

    Tua, shusha pumzi,

    Anza upya.