INDONESIA
Alithamini Utajiri wa Kiroho
Thio Seng Bie
-
ALIZALIWA 1906
-
ALIBATIZWA 1937
-
HISTORIA FUPI Mzee mwaminifu aliyevumilia jeuri ya kijamii.—Limesimuliwa na binti yake Thio Sioe Nio.
MWEZI Mei mwaka wa 1963, ghasia dhidi ya Wachina ziliibuka katika eneo la Java Magharibi. Jiji lililokumbwa na ghasia kubwa zaidi ni Sukabumi, ambako familia yetu ilifanya biashara. Watu wengi wenye fujo, hata majirani, walivamia nyumba yetu. Tulijawa na hofu walipovunja na kupora mali zetu.
Umati huo ulipoondoka, majirani zetu wengine walikuja kutufariji. Baba yangu aliketi pamoja nao sakafuni. Alichukua Biblia yake kubwa ya Kisunda katika mali zetu zilizoharibiwa. Aliifungua, akaisoma na kuwaeleza kwamba matatizo hayo yalitabiriwa. Kisha akawaeleza kwa shangwe kuhusu tumaini zuri la ufalme.
Kamwe, Baba yangu hakuwa na lengo la kujirundikia hazina duniani. Sikuzote alitukumbusha kwamba: “Mambo ya kiroho yanapaswa kutangulizwa!” Kwa sababu ya mfano wake mzuri, mke, watoto wake, baba yake mwenye umri wa miaka 90, na pia ndugu zake wengi wa ukoo na majirani walikubali kweli.