Matendo ya Mashahidi wa Yehova Katika Nyakati za Kisasa
Matendo ya Mashahidi wa Yehova Katika Nyakati za Kisasa
Kenya na Nchi Jirani
Kati ya sehemu zote za dunia, ni chache zilizo na msisimko, rangi, uzuri, na uvutano kama Mashariki mwa Afrika. Na ni watu wachache wameona watu ambao imani yao iliyotahiniwa imekuwa imara chini ya mnyanyaso mkali kama huo. Soma juu ya imani katika tendo nchini Kenya, Burundi, Djibouti, Ethiopia na Eritrea, Rwanda, Somalia, Sudan, Tanzania, na Uganda, kutia na Ushelisheli katika Bahari ya Hindi na Yemen kwenye Peninsula ya Uarabu.
Visiwa Solomoni
Lenye kuenea kama mikufu miwili ya lulu yenye thamani kwenye bahari ya Pasifiki ya rangi yenye feruzi mahali-mahali ni taifa la Kimelanesia la Visiwa Solomoni, ambavyo huitwa kwa upendo “Visiwa Vyenye Furaha” na wenyeji walo. Soma vile upendo wenye kina kirefu wa kueneza kweli ya Biblia umesaidia baadhi ya wenyeji wa kisiwa watimize mambo ya ajabu katika kufanya wanafunzi na kujenga majumba kwa ajili ya ibada ya Yehova Mungu.