Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Burudani

Burudani

SEHEMU YA 8

Burudani

Ni mara ngapi wewe hujifurahisha kwa mambo kama vile michezo, muziki, sinema, kutazama televisheni, au michezo ya kompyuta?

□ Mara chache sana

□ Mara moja kwa siku

□ Mara kadhaa kwa siku

Maamuzi yako kuhusu burudani hutegemea nani au nini hasa?

□ Vijana wenzako

□ Mzazi (wazazi) wako

□ Matangazo ya biashara

Tofauti na ilivyokuwa zamani, leo kuna tafrija nyingi zaidi ambazo wewe na vijana wenzako mnaweza kufurahia. Hata hivyo, bado siku zina saa 24 tu. Tafrija unayochagua inaweza kuathiri kufikiri kwako na mtazamo wako. Basi, ni kiasi gani cha wakati kinachofaa kutumiwa katika tafrija? Nawe unaweza kuamuaje tafrija inayofaa? Sura ya 30-33 zitakusaidia kufikiria kwa makini jinsi unavyochagua tafrija.

[Picha katika ukurasa wa 244, 245]