SWALI LA 4
Je, Uhai Wote Umetokana na Chanzo Kimoja?
Darwin alifikiri kwamba huenda uhai wote ulitokana na chanzo kimoja. Aliwazia kwamba historia ya uhai duniani inafanana na mti mkubwa. Baadaye, watu fulani waliamini kwamba huo “mti wa uhai” ulianza ukiwa shina moja lenye chembe sahili za kwanza. Spishi mpya zikachipuka kutoka katika shina na kuendelea kujigawanya kuwa viungo, au jamii za mimea na wanyama, na kisha machipukizi, yaani, spishi zote zilizopo leo katika jamii za mimea na wanyama. Kweli hivyo ndivyo ilivyokuwa?
Wanasayansi wengi husema nini? Wengi huhisi kwamba rekodi ya visukuku huunga mkono nadharia ya kuwapo kwa chanzo kimoja cha uhai. Pia, wanadai kwamba kwa kuwa vitu vyote vilivyo hai vinatumia “lugha ileile ya kompyuta,” au DNA, basi lazima uhai ulitokana na chanzo kimoja.
Biblia inasema nini? Masimulizi ya kitabu cha Mwanzo yanasema kwamba mimea, viumbe vya baharini, wanyama wa nchi kavu, na ndege viliumbwa “kulingana na aina yake.” (Mwanzo 1:12, 20-25) Masimulizi hayo yanaonyesha kwamba kuna unamna-namna katika “aina,” hata hivyo, yanamaanisha kwamba aina hizo mbalimbali zinatofautiana kabisa. Pia, masimulizi ya Biblia kuhusu uumbaji hutufanya tutazamie kwamba aina mpya za viumbe zingetokea ghafula katika rekodi ya visukuku zikiwa kamili.
Uthibitisho unafunua nini? Je, uthibitisho huo unaunga mkono masimulizi ya Biblia au Darwin alikuwa sahihi? Mavumbuzi ya miaka zaidi ya 150 iliyopita yamefunua nini?
MTI WA DARWIN WAKATWA
Katika miaka ya karibuni, wanasayansi wamefaulu kulinganisha chembe za urithi za viumbe mbalimbali wenye chembe moja na vilevile za mimea na wanyama. Waliamini kwamba kwa kufanya hivyo wanaweza kuthibitisha ule “mti wa uhai” wenye kutoa matawi uliopendekezwa na Darwin. Lakini, haijawa hivyo.
Utafiti umefunua nini? Mnamo 1999 mwanabiolojia Malcolm S. Gordon aliandika: “Inaonekana uhai ulikuwa na vyanzo vingi. Inaonekana chini ya ule mti wa uhai kulikuwa na mizizi mingi.” Kuna uthibitisho wowote kwamba yale matawi makuu ya uhai yanatoka katika shina moja, kama Darwin alivyoamini? Gordon aendelea: “Yaelekea ufafanuzi wa awali wa nadharia ya chanzo kimoja cha uhai haihusu himaya kama 29 *
zinavyotambuliwa leo. Huenda nadharia hiyo haihusu faila zote, na huenda pia haihusu matabaka ndani ya faila.”Utafiti wa karibuni unaendelea kupinga nadharia ya Darwin ya kuwapo kwa chanzo kimoja cha uhai. Kwa mfano, mwaka wa 2009, makala katika gazeti New Scientist ilimnukuu mwanasayansi wa mageuzi Eric Bapteste akisema: “Hatuna uthibitisho wowote kuonyesha kwamba mti wa uhai ni hakika.”30 Makala hiyohiyo inamnukuu mwanabiolojia wa mageuzi Michael Rose akisema: “Mti wa uhai unaendelea kuzikwa taratibu, sote twajua hilo. Kile tusichokubali hasa ni wazo la kwamba tunahitaji kubadili maoni yetu yote kuhusu biolojia.”31 *
NAMNA GANI REKODI YA VISUKUKU?
Wanasayansi wengi huona rekodi ya visukuku kuwa inaunga mkono dhana ya kwamba uhai ulitokana na chanzo kimoja. Kwa mfano, wao hudai kwamba rekodi ya visukuku huonyesha kwamba samaki waligeuka na kuwa amfibia na reptilia wakawa mamalia. Hata hivyo, visukuku huthibitisha nini hasa?
Mwanamageuzi ambaye pia ni mtaalamu wa visukuku, David M. Raup anasema: “Badala ya kuchunguza jinsi uhai ulivyotokea hatua kwa hatua, kile ambacho wanajiolojia wa siku za Darwin na wa leo wanapata ni rekodi isiyolingana au isiyo na mpangilio; kwamba spishi zinaonekana ghafula kwa mfuatano, zinakuwa na mabadiliko madogo au hata bila mabadiliko yoyote, kisha zinatoweka ghafula kutoka katika rekodi.”32
Kusema kweli, visukuku vingi huonyesha kwamba aina tofauti-tofauti za viumbe hazijabadilika hata baada ya muda mrefu sana. Uthibitisho hauonyeshi vikigeuka kutoka kwa aina moja hadi nyingine. Maumbo ya kipekee hutokea ghafula. Sehemu mpya hutokea ghafula. Kwa mfano, popo wenye mfumo wa sona ambao wana uwezo wa kugundua mahali kitu fulani kinapatikana kwa kutumia mawimbi ya sauti, hawana uhusiano ulio wazi na popo wa kale.
Inaonekana zaidi ya nusu ya vikundi vyote vikuu vya wanyama vilitokea kwa muda mfupi wa wakati. Kwa kuwa aina nyingi mpya za uhai zinazotofautiana sana zinatokea ghafula kwenye rekodi ya visukuku, wataalamu wa visukuku hukiita kipindi hicho “mlipuko wa Cambria.” Huo ulikuwa wakati gani?
Tuchukulie kwamba makadirio ya watafiti ni sahihi. Hivyo basi, historia ya dunia inaweza kuwakilishwa na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha wakati kinachoweza kunyooshwa na kutoshana na uwanja wa mpira wa kandanda (1). Kwa kipimo hicho, utahitaji kutembea asilimia 88 ya uwanja huo kabla ya kufikia kile ambacho wataalamu wa visukuku wanakiita kipindi cha Cambria (2). Katika muda mfupi wa kipindi hicho, vikundi vikubwa vya wanyama vinaonekana katika rekodi ya visukuku. Vinatokea ghafula kadiri gani? Unapoendelea kutembea kwenye uwanja huo, viumbe vyote hivyo tofauti-tofauti vinatokea upesi kwa muda unaopungua hatua moja!
Kutokea ghafula kwa aina hizo tofauti-tofauti za uhai kumefanya watafiti fulani wa nadharia ya mageuzi kutilia shaka masimulizi ya jadi ya nadharia ya Darwin. Kwa 33
mfano, kwenye mahojiano ya mwaka 2008, mwanamageuzi, Stuart Newman, alizungumzia uhitaji wa kuwa na nadharia nyingine ya mageuzi inayoweza kufafanua kutokea ghafula kwa aina mpya mbalimbali za uhai. Alisema: “Nadharia ya Darwin iliyokuwa ikifafanua mabadiliko yote ya mageuzi itashushwa, iwe tu kama mojawapo ya nadharia nyingi—huenda hata isiyo muhimu sana inapohusu kuelewa mageuzi makubwa, mageuzi ya mabadiliko makubwa katika maumbo ya mwili.”MATATIZO YA “UTHIBITISHO”
Hata hivyo, namna gani visukuku vinavyotumiwa kuonyesha samaki wakibadilika kuwa amfibia, na reptilia kuwa mamalia? Je, vinaandaa uthibitisho thabiti kuhusu hatua za mageuzi? Rekodi ya visukuku inapochunguzwa kwa makini, matatizo mengi huwa wazi.
Kwanza, nyakati nyingine ukubwa wa viumbe katika mfuatano wa mabadiliko kutoka reptilia-hadi-mamalia hupotoshwa katika vitabu. Badala ya kuwa sawa kwa ukubwa, viumbe fulani katika mfuatano huwa vikubwa, huku vingine vikiwa vidogo.
Pili, tatizo kubwa hata zaidi ni ukosefu wa uthibitisho unaoonyesha kwamba viumbe hao wanahusiana kwa njia fulani. Kulingana na makadirio ya watafiti, mara nyingi wanyama walio kwenye mfuatano hutenganishwa na mamilioni ya miaka. Kuhusiana na wakati unaotenganisha visukuku hivyo, mwanazuolojia Henry Gee anasema: “Muda unaotenganisha visukuku ni mrefu sana hivi kwamba hatuwezi kusema kwa uhakika ikiwa vinahusiana kupitia nasaba na ukoo.”34 *
Akizungumzia visukuku vya samaki na amfibia, mwanabiolojia Malcolm S. Gordon, anasema kwamba visukuku vilivyopatikana vinawakilisha sehemu ndogo tu “huenda isiyowakilisha kabisa aina mbalimbali ya mimea na wanyama 35 *
waliokuwako katika vikundi hivyo wakati huo.” Anaendelea kusema: “Hatuwezi kujua ni kwa kiasi gani viumbe hao walihusika katika ukuzi wa baadaye, au jinsi walivyohusiana.”“FILAMU” INAONYESHA NINI HASA?
Makala iliyochapishwa mwaka wa 2004 katika jarida la National Geographic lilifananisha rekodi ya visukuku na “filamu ya mageuzi ambayo kati ya kila picha 1,000, imepoteza picha 999 katika chumba cha kuhariri.”36 Fikiria matokeo ya mfano huo.
Wazia umepata picha 100 ya filamu ambayo mwanzoni ilikuwa na picha 100,000. Utajuaje mfuatano wa matukio katika filamu hiyo? Huenda ukawa na maoni fulani, lakini namna gani ikiwa ni 5 tu kati ya zile picha 100 ulizopata zinazoweza kupangwa ili kuunga mkono hadithi unayopendelea, huku zile nyingine 95 zikiwa na hadithi tofauti? Lingekuwa jambo la hekima kudai kwamba maoni yako kuhusu filamu hiyo ni sahihi kwa sababu tu ya hizo picha tano? Inawezekana kwamba uliweka picha hizo tano kwa mpangilio ambao unapatana na maoni yako? Je, halingekuwa jambo la busara kuacha zile picha nyingine 95 zikusaidie kuwa na maoni yanayofaa?
Ni kwa njia gani mfano huo unatusaidia kuelewa jinsi wanamageuzi wanavyoiona rekodi ya visukuku? Kwa miaka mingi, watafiti hawakukubali kwamba visukuku vingi—zile picha 95 za filamu—vilionyesha kwamba spishi hubadilika kidogo sana baada ya muda. Kwa nini hawasemi lolote kuhusu uthibitisho huo muhimu? Mwandikaji Richard Morris anasema: “Yaelekea wataalamu wa visukuku walianza kushikilia maoni yaliyokubaliwa na wengi kwamba kulikuwa na mabadiliko ya hatua kwa hatua katika mageuzi, hata baada ya kupata uthibitisho unaokanusha jambo hilo. Wamekuwa 37
wakijaribu kufafanua uthibitisho wa visukuku kulingana na maoni yanayokubaliwa kuhusu mageuzi.”“Kuchukua visukuku kadhaa na kudai kwamba vinawakilisha nasaba fulani si maoni ya sayansi yanayoweza kuthibitishwa, balini dai linaloweza kulinganishwa na hadithi zinazosimuliwa kabla ya kulala—zinazosisimua, huenda hata zenye mafunzo, lakini zisizo za kisayansi.”—In Search of Deep Time—Beyond the Fossil Record to a New History of Life, cha Henry Gee, uku. 116-117
Namna gani wanamageuzi leo? Inawezekana kwamba wanapanga visukuku katika mpangilio fulani, si kwa sababu mfuatano huo unaungwa mkono na visukuku vingi na uthibitisho wa kinasaba, bali kwa sababu kufanya hivyo kunapatana na maoni yanayokubaliwa leo kuhusu mageuzi? *
Una maoni gani? Ni kauli gani inayopatana kabisa na uthibitisho? Fikiria ukweli wa mambo ambao tumezungumzia kufikia sasa.
-
Uhai wa kwanza duniani haukuwa “duni.”
-
Uwezekano wa hata visehemu vya chembe kujitokeza vyenyewe ni mdogo sana.
-
DNA, “programu ya kompyuta,” au mfumo, huendesha chembe, nayo ni tata sana na ina uwezo wa hali ya juu sana kupita programu au mfumo wowote wa kuhifadhi habari ambao umewahi kutengenezwa na mwanadamu.
-
Utafiti wa kinasaba umeonyesha kwamba uhai haukutokana na chanzo kimoja. Isitoshe, vikundi vikubwa vya wanyama huonekana ghafula katika rekodi ya visukuku.
Baada ya kuchunguza ukweli huo, je, unafikiri inafaa kukata kauli kwamba uthibitisho huo unapatana na masimulizi ya Biblia kuhusu chanzo cha uhai? Hata hivyo, watu wengi hudai kwamba sayansi hupinga mambo mengi ambayo Biblia husema kuhusu uumbaji. Je, ni kweli? Biblia husema nini hasa?
^ fu. 9 Neno la kibiolojia faila linarejelea kikundi kikubwa cha wanyama wenye sifa zinazofanana. Njia moja ambayo wanasayansi huainisha vitu vyote vilivyo hai ni kwa kutumia mfumo wa hatua saba, ambapo kila hatua iko wazi zaidi kuliko ile inayoitangulia. Hatua ya kwanza ni himaya, ambayo ndiyo kikundi kikubwa zaidi. Kisha faila, tabaka, oda, jamii, jenasi, na spishi. Kwa mfano, farasi ameainishwa kwa njia ifuatayo: himaya, Animalia; faila, Kodata; tabaka, Mamalia; oda, Perissodactyla; jamii, Equidae; jenasi, Equus; spishi, Caballus.
^ fu. 10 Kumbuka kwamba wala makala ya gazeti la New Scientist, wala maoni ya Bapteste, wala ya Rose, hayadokezi kwamba nadharia ya mageuzi si ya kweli. Badala yake, wanachosema ni kwamba ule mti wa uhai wa Darwin ambao ndiyo msingi wa nadharia yake, haungwi mkono na uthibitisho. Wanasayansi kama hao bado wanatafuta njia nyingine ya kufafanua nadharia ya mageuzi.
^ fu. 21 Henry Gee hadokezi kwamba nadharia ya mageuzi si ya kweli. Maelezo yake yamekusudiwa kuonyesha kwamba watu hawawezi kujifunza mengi kutokana na visukuku.
^ fu. 22 Malcom S. Gordon anaunga mkono fundisho la mageuzi.
^ fu. 27 Kwa mfano, ona sanduku “Namna Gani Mageuzi ya Mwanadamu?”
^ fu. 50 Kumbuka: Hakuna yeyote kati ya watafiti wanaonukuliwa katika sanduku hili anayeamini mafundisho ya Biblia kuhusu uumbaji. Wote wanaunga mkono mageuzi.
^ fu. 54 Neno “hominidi” linatumiwa kufafanua kile ambacho watafiti wa mageuzi huona kuwa kinafanyiza jamii ya mwanadamu na spishi za viumbe wengine wa kale wanaofanana na mwanadamu.