SEHEMU YA 2
Gharika Mpaka Kukombolewa Katika Misri
Watu wanane peke yao ndio waliookoka Gharika, lakini baadaye wakaongezeka kuwa maelfu mengi. Kisha, ilipopita miaka 352 baada ya Gharika, Abrahamu akazaliwa. Tunajifuzna namna Mungu alivyotimiza ahadi yake kwa kumpa Abrahamu mwana anayeitwa Isaka. Kisha, kati ya wana wawili wa Isaka, Yakobo alichaguliwa na Mungu.
Yakobo alikuwa na jamaa kubwa ya wana 12 na binti fulani. Wana 10 wa Yakobo walimchukia ndugu yao mdogo Yusufu wakamwuza utumwani huko misri. Baadaye, Yusufu akawa mtawala mkuu wa Misri. Njaa kuu ilipotokea, Yusufu aliwajaribu ndugu zake aone kama wamegeuza moyo. Halafu, jamaa yote ya Yakobo, yaani, Waisraeli, wakahamia Misri. Hayo yalitokea miaka 290 baada ya kuzaliwa Abrahamu.
Kwa miaka 215 iliyofuata Waisraeli walikaa huko Misri. Yusufu alipokufa, wakawa watumwa huko. Mwishowe, Musa akazaliwa, naye Mungu akamtumia awakomboe Waisraeli kutoka Misri. Kwa jumla, miaka 857 ya historia inazungumziwa katika Sehemu ya 2.
KATIKA SEHEMU HII
HADITHI YA 12
Watu Wanajenga Mnara Mkubwa
Mungu hakupendezwa, na adhabu aliyotoa bado huwaathiri wanadamu hadi leo.
HADITHI YA 13
Ibrahimu—Rafiki ya Mungu
Kwa nini Ibrahimu aliacha makao yake ya starehe na kuanza kuishi katika mahema?
HADITHI YA 14
Mungu Anajaribu Imani ya Ibrahimu
Kwa nini Mungu alimwomba Ibrahimu amtoe mwana wake Isaka kuwa dhabihu?
HADITHI YA 16
Isaka Anapata Mke Mzuri
Ni nini kilichofanya Rebeka awe mke mzuri? Je, ni urembo au ni jambo lingine?
HADITHI YA 17
Mapacha Waliokuwa Tofauti
Baba yao, Isaka, alimpenda sana Esau, lakini mama yao Rebeka, alimpenda sana Yakobo.
HADITHI YA 19
Yakobo Ana Jamaa Kubwa
Je, majina ya makabila 12 ya Israeli yalitokana na wana 12 wa Yakobo?
HADITHI YA 21
Yusufu Anachukiwa na Ndugu Zake
Ni nini kiliwachochea baadhi yao watake kumuua ndugu yao?
HADITHI YA 22
Yusufu Anawekwa Katika Gereza
Afungwa gerezani, si kwa sababu alivunja sheria, lakini kwa sababu alifanya yaliyo sawa.
HADITHI YA 24
Yusufu Anajaribu Ndugu Zake
Atajuaje ikiwa wamebadilika tangu walipomuuza kama mtumwa?
HADITHI YA 26
Ayubu ni Mwaminifu kwa Mungu
Ayubu alipoteza mali, afya, na watoto. Je, Mungu alikuwa akimwadhibu?
HADITHI YA 27
Mfalme Mbaya Anatawala Misri
Kwa nini aliamuru watu wake wawaue watoto wote wa kiume wa Waisraeli?
HADITHI YA 28
Namna Mtoto Musa Alivyookolewa
Mama yake alitafuta njia ya kukwepa amri iliyoamuru watoto wavulana wa Waisraeli wauawe.
HADITHI YA 29
Sababu Musa Alikimbia
Musa alifikiria kwamba alikuwa tayari kuwaokoa Waisraeli alipokuwa na umri wa miaka 40, lakini hakuwa tayari.
HADITHI YA 30
Mti Mdogo Unaowaka
Kwa kutumia mfuatano wa miujiza, Mungu anamwambia Musa muda umefika wa Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri.
HADITHI YA 31
Musa na Haruni Wanamwona Farao
Kwa nini Farao hamsikilizi Musa na kuwaachilia Waisraeli?
HADITHI YA 32
Mapigo 10
Mungu alileta mapigo kumi kwa sababu Farao, mtawala wa Misri kwa kiburi aliwakataza Waisraeli wasiondoke.
HADITHI YA 33
Kuvuka Bahari Nyekundu
Musa atenganisha Bahari Nyekundu kwa nguvu za Mungu na Waisraeli wavuka na kwenda nchi kavu.