Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HADITHI YA 20

Dina Anaingia Katika Taabu

Dina Anaingia Katika Taabu

UNAONA Dina anaenda kutembela nani? Ni wasichana wanaokaa Kanaani. Je! Yakobo baba yake atafurahia? Ili uweze kujibu ulizo hilo, jaribu kukumbuka Ibrahimu na Isaka walivyofikiria wanawake wa Kanaani.

Je! Ibrahimu alitaka Isaka aoe msichana wa Kanaani? Sivyo. Je! Isaka na Rebeka walitaka Yakobo aoe msichana wa Kanaani? Sivyo. Unajua sababu yake?

Ni kwa sababu watu hao wa Kanaani waliabudu miungu ya uongo. Hawakufaa kuwa waume wa wake, nao hawakufaa kuwa rafiki wa kushirikiana nao. Basi tunaweza kuwa na hakika kwamba Yakobo hangependezwa na urafiki wa binti yake pamoja na wasichana hao Wakaanani.

Bila shaka, Dina aliingia katika taabu. Je! unamwona mwanamume huyo Mkanaani katika picha anayemtazama Dina? Ni Shekemu. Siku moja Dina alipokuwa akitembelea, Shekemu alimchukua na kumlazimisha alale naye. Hilo lilikuwa kosa, kwa sababu ni wanaume na wanawake waaliooana tu ndio wanaotakiwa kulala pamoja. Ubaya huo ambao Shekemu alimtemtendea Dina uliongoza kwenye taabu nyingi zaidi.

Ndugu zake Dina waliposikia yaliyotokea, walikasirika sana. Simeoni na Levi, walikasirikika sana hata wakachukua panga wakaingia mjini na kuwafikia wanaume hao ghafula. Wao na ndugu zao wakamwua Shekemu na wanaume wengine wote. Yakobo alikasirika kwa sababu wanawe walifanya ubaya huo.

Taabu yote hiyo ilianza namna gani? Ni kwa sababu Dina alifanya urafiki na watu ambao hawakutii sheria za Mungu. Hatutaki tufanye urafiki na watu kama hao, sivyo?