SEHEMU YA 3
Kukombolewa Misri Mpaka Mfalme wa Kwanza wa Israeli
Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka utumwa wa Misri kwenda kwenye Mlima Sinai, ambako Mungu aliwapa sheria zake. Baadaye, Musa akawatuma wanaume 12 wakapeleleze nchi ya Kanaani. Lakini 10 kati yao wakarudisha ripoti mbaya. Waliwafanya watu watake kurudi Misri. Kwa kukosa imani, Mungu aliwaadhibu Waisraeli kwa kuwafanya watange-tange jangwani muda wa miaka 40.
Mwishowe, Yoshua akachaguliwa aongoze Waisraeli kuingia nchi ya Kanaani. Ili kuwasaidia waichukue nchi hiyo Yehova alifanya miujiza mingi. Alifanya maji ya Mto Yordani yaache kutiririka, kuta za Yeriko zianguke, jua lisimame bila kwenda kwa siku nzima. Baada ya miaka sita, nchi hiyo ikachukuliwa kutoka kwa Wakanaani.
Kuanzia na Yoshua, Waisraeli walitawalwa na mahakimu (waamuzi) muda wa miaka 356. Twajifunza habari za wengi wao, kutia Baraki, Gideoni, Yeftha, Samsoni na Samweli. Pia twasoma habari za wanawake kama Rahabu, Debora, Yaeli, Ruthu, Naomi na Delila. Kwa jumla, Sehemu ya 3 inasimulia historia ya miaka 396.
KATIKA SEHEMU HII
HADITHI 38
Wapelelezi 12
Wapelelezi kumi wanasema jambo moja, na wawili jambo tofauti. Waisraeli wanawaamini nani?
HADITHI YA 48
Wagibeoni Wenye Hekima
Walimdanganya Yoshua na Waisraeli ili wawape ahadi, hata hivyo Waisraeli walitimiza ahadi yao.
HADITHI YA 49
Jua Linasimama Tu
Yehova anamfanyia Yoshua jambo ambalo hakuwahi kufanya na hajawahi kufanya tena tangu wakati huo.
HADITHI 50
Wanawake Hodari Wawili
Baraki anaongoza jeshi la Waisraeli vitani, hivyo kwa nini Yaeli anasifiwa?
HADITHI 55
Mvulana Mdogo Anamtumikia Mungu
Mungu anamtuma Samweli kumwambia Kuhani Mkuu Eli ujumbe mzito.